Wandishi wa Sweden wahukumiwa
21 Disemba, 2011 - Saa 16:59 GMT
Mahakama ya nchini Ethiopia
imewapata na hatia wandishi habari wawili kutoka Sweden ya bkuunga mkono
kundi la kigaidi. Upande wa mashtaka umeomba wapewe hukumu ya kifungo
cha zaidi ya miaka 18.
Makundi yanayotetea haki za binadamu yamekashifu uwamuzi wa Mahakama ya Ethiopia.
Akiwasilisha hukumu yake, Jaji Shemsu Sirgaga amesema kua Martin Schibbye na Johan Persso wameonyesha kua walikua waandishi mashuhuri lakini akaongezea kua hawakuweza kuthibitisha kua hawaungi mkono ugaidi.
Kundi la wandishi habari linalotetea Uhuru wa uandishi habari, Reporters without borders, limelaani uwamuzi wa Jaji huyo uliobaini ukakamavu wa viongozi wa Ethiopia. Kundi hilo limesema kua badala ya uwamuzi kubaini makosa ya wandishi hao limewatuhumu kwa kushindwa kujitetea.
Mwezi Julai uliopita wandishi hao wawili kutoka Sweden walikamatwa na Jeshi la Ethiopia baada ya mapambano na waasi wa Ogaden ONLF.
Walikua pamoja na waasi lakini wakakanusha kua walishiriki mbali na kazi yao kama wandishi wa habari...walisema kua walikua wakikusanya taarifa kuhusu shuughuli za kampuni ya mafuta ya Sweden katika eneo hilo.
Martin Schibbye na Johan Persson walikiri kua kweli waliingia nchi bila kibali. Serikali ya Ethiopia hairuhusu mtu kuingia eneo la Ogaden ambako zimetokea habari za ukiukaji wa haki za binadamu zinazofanywa na serikali hio katika jitihada yake ya kulizima kundi hilo la waasi.
Kamati ya shirika linalohusika na usalama wa wandishi wa habari inasema kua ingawa Ethiopia hupokea msaada mkubwa wa kigeni lakini nchi hio imezidi kua msitari wa mbele katika unyanyasaji ikiwa mojapo ya nchi zenye wandishi wa habari walioikimbia nchi yao.
No comments:
Post a Comment