Sunday, December 4, 2011

Baada ya Kyoto itakuwaje?


Baada ya Kyoto

 4 Disemba, 2011 - Saa 12:36 GMT
Mawaziri wanatarajiwa kuanza kuwasili leo kwenye mkutano wa mwaka wa Umoja wa Mataifa kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa, unaofanywa Durban, Afrika Kusini.
Mabadiliko ya hali ya hewa
Maelfu ya waandamanaji wamekuwa mitaani wakidai viongozi wa kimataifa wachukue hatua.
Nchi kadha maskini zinasema zinataka mkataba mpya wa kimataifa, utaochukua nafasi ya muafaka wa Kyoto ambao utamalizika mwakani.
Lakini baadhi ya mataifa - ikiwemo Marekani, Canada na Saudi Arabia - yanataka mkataba mpya uakhirishwe hadi angalau mwaka wa 2015.
Dakta Paula Owen ni mshauri wa maswala ya nishati na mabadiliko ya hali ya hewa.
Anasema mkutano huo ni muhimu:
"Ulioko sasa ni muafaka wa Kyoto ambao unalazimisha nchi za dunia nzima kupunguza kiwango cha gesi inayozidisha joto duniani.
Tatizo ni kuwa utamalizika mwisho wa mwaka 1212, na hivi sasa hakuna makubaliano mengine ya kuchukua nafasi yake."

No comments:

Post a Comment