Wednesday, December 28, 2011

Korea Kaskazini yafanya maziko ya Kim Jong -il


Korea Kaskazini yafanya maziko ya Kim Jong -il

 28 Disemba, 2011 - Saa 07:22 GMT
Maiti ya Kim Jong-Il
Korea Kaskazini inafanya maziko ya kitaifa ya kiongozi wake Kim Jong-il huku msafara mkubwa wa magari yaliyosindikiza jeneza la kiongozi huyo ukipitia mji mkuu Pyongyang.
Picha cha runinga zimeonyesha maelfu ya wanajeshi wakitoa heshima za mwisho kwa picha ya kiongozi huyo iliyopitia kwenye barabara za mji.
Mridhi wa uwongozi ambaye ni mwanawe wa kiume Kim Jong-Un amezindikisha jeneza la babake lililokuwa juu la gari maalum. Kim Jong-il alifariki dunia Decemba 17 baada ya kupatwa na mshtuko wa moyo akiwa na miaka 69.
Hakuna viongozi wa nje walioalikwa wala waandishi wa habari wa kimataifa. Wadadisi wanasema mazishi ya leo ni sambamba na ya mwasisi wa nchi hiyo Kim IL-Sung mwaka 1994 yalioandamana na gwaride kubwa ya kijeshi.
Kiongozi mtarajiwa Kim Jon-Un ameandamana na mjombake Chang Song-taek anayetarajiwa kuwa na ushawishi mkubwa katika uwongozi mpya pia mkuu wa jeshi Ri Yong-ho, alionekana kando ya jeneza la Kim Jong-Il.
Kabla ya kufariki kiongozi wa Korea Kaskazini alikuwa katika mchakato wa kumtayarisha mwanawe Kim Jong-Un kuchukua hatamu za uwongozi. Kifo chake cha ghafla cha Kim Jong Il kimepelekea hofu ya kuzuka mzozo wa uwongozi katika taifa hilo lenye msingi wa ujamaa

No comments:

Post a Comment