Laurent Gbagbo kufika mbele ya ICC
5 Disemba, 2011 - Saa 03:28 GMT
Rais aliyeondolewa madarakani
nchini Ivory Coast Laurent Gbagbo anafikishwa mbele ya mahakama ya
kimataifa ya Jinai ICC hii leo. Mwansiasa huyo anatarajiwa kufunguliwa
mashtaka ya uhalifu wa kivita. Gbagbo alipelekewa nchini Uholanzi wiki
jana.
Mahakama ya ICC imemtuhumu Gbagbo kwa makosa ya
uhalifu wa kivita kufuatia machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa Ivory
Coast mwaka jana alipopinga kuyakabidhi madaraka kwa mpinzani
wake,Alassane Ouattara, ambaye sasa ndiye rais wa Ivory Coast.Kiongozi huyo ambaye ndiye rais wa kwanza kufikishwa mbele ya ICC atasomewa makosa yake chini ya sheria za mkataka wa Roma uliounda mahakama hiyo. Baada ya kusomewa mashtaka yake itakuwa jukumu la majaji waandamizi kuamua siku ya kusikizwa kwa kesi dhidi ya Laurent Gbagbo.
Iran yadungua ndege ya Marekani
Jeshi la Iran linasema ndege yenyewe haikuwa na rubani
No comments:
Post a Comment