Tshisekedi aonywa asijitangaze Rais
19 Disemba, 2011 - Saa 03:52 GMT
Serikali ya Jamhuri ya
Kidemokrasi ya Congo imeonya kumchukulia hatua kali kiongozi wa upinzani
Etienne Tshisekedi kwa kujitangaza kuwa yeye ndiye Rais mpya wa taifa
hilo.
Akihutubia mkutano wa waandishi wa habari mjini Kinshasa Jumapili, Tshisekedi alisema: "Naamuru maafisa wote wa jeshi na polisi kutii utawala wa kweli uliochaguliwa na Congo. Waache kutii watu ambao kesho watajieleza kwa mahakama za kitaifa na kimataifa kwa makosa waliyofanya wakati wa kutawala taifa hili."
Bwana Tshisekedi alitangazwa kuwa wa pili katika uchaguzi wa Urais akimfuatia Rais Joseph Kabila. Mahakama ya juu nchini humo pia ilithibitisha kuwa Rais Kabila ndiye aliyeshinda uchaguzi huo.
Tangu kampeni za uchaguzi wa Urais kuanza miezi miwili iliyopita na kisha kura kupigwa na kutangazwa na tume ya uchaguzi Tshisekedi amejitangaza mara tatu sasa kuwa ndiye Rais.
No comments:
Post a Comment