Monday, December 19, 2011

Rambi rambi juu ya kifo cha Havel

Rambi rambi juu ya kifo cha Havel

 18 Disemba, 2011 - Saa 16:40 GMT
Wananchi wa Uczech na wanasiasa wamejumuika na viongozi wa kimataifa kueleza heshima zao kwa Vaclav Havel.
Vaclav Havel
Bendera nyeusi imepepea ikulu mjini Prague.
Vaclav Klaus, ambaye alirithi kiti cha rais kutoka Havel, alimuelezea aliyemtangulia kuwa alama ya enzi mpya ya taifa la Czech.
Chancellor Angela Merkel wa Ujerumani alisema Wajerumani wanamshukuru kwa mengi, na watamkumbuka kwa kutetea uhuru na demokrasi na kwa utu wake.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, alisema Vaclav Havel aliwaongoza watu wa Czech kutoka kwenye udikteta.

No comments:

Post a Comment