Saturday, December 3, 2011

PAPA BENEDICT AUSHTUA ULIMWENGU


Papa Benedict XVI.
Hamida Hassan na Mitandao
KIONGOZI Mkuu wa Kanisa Katoliki duniani, Joseph Aloisius Ratzinger ‘Papa Benedict XVI’, ameushtua ulimwengu, ishara ya vidole na mikono wakati wa kutoa salamu katika picha zilizotundikwa mitandaoni, vimefananishwa na alama za Jamii ya Siri (Secret Society) inayoitwa Freemasons.

Tony Blair akisalimiana na Papa.
 
Zipo taarifa kuwa Freemasons kwa sehemu kubwa wanamuabudu Shetani (Jini Mkuu) anayeitwa Lucifer ndiyo maana imekuwa ikiitwa Dini ya Shetani.

Wachambuzi wa mambo ya Freemasons wanaeleza kuwa jamii hiyo ya siri inapiga vita Uislam na Ukristo hali ambayo imeibua mshtuko baada ya picha hizo kumuonesha Papa Benedict akitumia alama za watu ambao ni maadui wa madhehebu anayoyaongoza.


Picha zilizoibua maswali na mshtuko, moja inamuonesha Papa akiwa anatoa salamu ya vidole ambavyo amevitengeneza kama pembe ya mbuzi, nyingine akiwa anapeana mikono na Waziri Mkuu Mstaafu wa Uingereza, Tony Blair.

Inadaiwa kuwa mtindo wa kupeana mikono walioutumia Blair na Papa, si wa kawaida, kwani mara nyingi hutumiwa na memba wa Freemasons wanaposalimiana au kupongezana.

Barack Obama.

MASWALI TATA
Kutokana na picha hizo za Papa, imeibuka mijadala mingi mitandaoni kuhusu imani ya kiongozi huyo wa Kanisa Katoliki lakini mwisho kumekuwa na maswali matano ambayo yamekosa majibu:

MOSI: Papa Benedict ni Freemason?
PILI: Ni mfuasi wa jamii inayopingana na maono ya kanisa analoongoza?

TATU: Kama siyo Freemason, je, anawakubali na kuwasapoti?
NNE: Je, alitoa salamu bila kujua maana yake?
TANO: Papa alitumia salamu hiyo kumkejeli Shetani ambaye ndiye mkuu wa Freemasons?

http://www.jesus-is-savior.com/False%20Religions/Wicca%20&%20Witchcraft/bush_satan_sign.jpg
George W. Bush.

WAKATOLIKI WALAANI
Kwa mujibu wa maelezo ya watu ambao wamejipambanua kwamba ni waumini wa madhehebu ya Kanisa Katoliki, picha hizo zenye ishara ya vidole vya ki-Freemasons, zimetengenezwa kwa lengo la kuwafanya Wakatoliki watilie shaka mwenendo wa kiongozi wao.

Rahel Ratzega aliyejitambulisha kuwa ni Mkatoliki, raia wa Sweden alisema wakati anachangia habari ya Papa na vidole vya ki-Freemasons: “Mimi ni mtaalamu wa kompyuta, picha ya Papa imewekewa vidole vya mfuasi wa Freemasons ili kutuchafua Wakotiliki.

http://files.myopera.com/philiconvallley/albums/8711752/thumbs/hillary%20clinton%20freemasons.jpg_thumb.jpg
Hillary Clinton.
 
“Mimi na Wakatoliki wenzagu wa kanisa letu la Nytorv Square tumelaani hili, tumeujua ukweli kwamba picha ya Papa imetengenezwa. Tunaamini Freemasons ndiyo waliotengeneza ili kuwafanya Wakatoliki waone kiongozi wao ni mfuasi wa imani zenye mrengo wa Shetani.

“Tunamuamini Mungu, Shetani hayupo na sisi. Freemasons ni maadui wa Wakatoliki.”
Kuhusu picha ya Papa kushikana mikono na Blair, imeelezwa kuwa kiongozi huyo alitegwa.

Margaret Ryan, aliyejitambulisha kuwa ni Mkatoliki anayesali kanisa lililopo Newington, London, England, alisema: “Tunamtambua Blair ni Freemason, kwa hiyo alichokifanya ni kumtegea mkono Papa.

Sarkozy na Gaddafi wakisalimiana kwa ishara za Freemason.

“Papa siyo Freemason, Blair alimfanyia usanii Papa, akampa mkono kwa mtindo wa Freemason, bila kujua Papa naye akakubali mkono wake kumbe kwa mwenzake hiyo ina maana kubwa.

“Blair ni mmoja wa waumini wa Freemasons wenye digrii za juu kabisa, hata ule mtego wake kwa Papa haukuwa wa hivi hivi, lengo lake lilikuwa ni kuukejeli Ukatoliki kwa sababu Blair mbali na Freemason pia anaabudu Anglikana.”

Hata hivyo, wamiliki wa mtandao uliochapisha picha hizo walisisitiza kuwa ni halisi na hazifanyiwa utundu wowote wa kikompyuta.

Bill Clinton.
 
FREEMASONS INAZIDI KUPATA UMAARUFU
Hivi karibuni Freemasons imekuwa ikipata umaarufu mkubwa huku watu wakifurika huko na wasiojua chochote juu ya dini hiyo wameendelea kusaka kuijua kiundani.
Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!

Join Global Publishers
sophy Comment by sophy yesterday
Hapa Papa ndio mwenye ukweli juu ya mambo kama kweli au la.  Ila kama ni kweli atakuwa anamdhihaki mwenyezi mungu.  kinachonichanganya mie katika hali ya kawaida kukunja hivyo vidole kama hujazowea ni kazi kweli kweli hapa kidogo naona kunautata.
abdullah Nassor Comment by abdullah Nassor yesterday
wote inzi hujui dike wala dume.
sakina  shabani Comment by sakina shabani yesterday
Dini ya kweli huwezi ukamlazimisha mtu kuifata,wanaomuabudu shetani na wao ni  mashetan coz wanamkubali.ila mkumbuke ya kwamba shetani kalaaniwa na mwenyezi mungu kutokana na kutotii amri zake.hiyo ni audhubillah minasheitwan rajjim.
irene mhina Comment by irene mhina yesterday
tusiyumbishwe na mambo ya ajabu jamani, hata kama kaonyesha kweli inahusiana nini na imani yako? kwa ujinga ndio utasema papa anakupotosha, lakini yeye hajawahi hata siku moja kusema ni free watever,,, tuwe na misimamo unless otherwise tutashindwa kuendelea tutabaki kushabikia mambo ya kijinga ti
Nicolao Comment by Nicolao on Thursday
Ni ujinga , Freemasons wasijidai, huko ni kupumbaza umma wa Yesu, ni njama za shetan tu tumezigundua
vicque jonathan Comment by vicque jonathan on Thursday
mimi naona hapo papa hakujua maana ya hiyo salamu, na pia hapo yeye alisalimia tu na sivinginevyo mnavyofikiria nyinyi, hii freemasons ni nini hasa mbona watu hamna imani jamani?? kumbuka imani yako ndiyo itakayokuponya
Mia andy Comment by Mia andy on Tuesday
ndani ya marekani kwenye sign language(lugha ya ishara za mikono itumiwayo na viziwi na ma-bubu)
kufanya mkono kama hizo picha zinavyoonyesha ina maananisha kuwa nakupenda,nawapenda au nawajali n.k. Ni kama ile alama ya vidole wanayoitumia CHADEMA huku maana yake ni peace yaani amani
bongo Comment by bongo on Monday
Namshukuru mwenyezi mungu kwa kuzaliwa muisilamu.Dini yenye muongozo wa haki na yenye kumlaani shetani usiku na mchana.
Islam is the only way of life.
Very proud.
chalz Comment by chalz on Monday
Hawana lolote, hata wao wanajua YESU ni nani. NI BWANA NA MWOKOZI WA MAISHA YETU. Watashindwa 2 na freemasons yao.
Sixbert Comment by Sixbert on Monday
...yote haya yalishatabiriwa....wataibuka wengi kumpinga Mungu wa kweli,,,,picha zimetengenezwa ili kuangusha imani za watu....HATUDANGANYIKI!!!!!!!!!!

No comments:

Post a Comment