Monday, December 26, 2011

Papa Benedict alaani ghasia za Nigeria


Papa Benedict alaani ghasia za Nigeria

 25 Disemba, 2011 - Saa 16:17 GMT
Vatikani imelaani miripuko iliyotokea kwenye kanisa, Abuja, kuwa kitendo cha vipofu, wajinga na magaidi wanaochochea chuki.
Mti wa Krismasi katika medani ya St Peter's, Vatikani
Katika ujumbe wake wa Krismasi katika medani ya St Peter's, Vatikani, Papa Benedict piya alitoa wito umwagaji damu usite nchini Syria, na mazungumzo ya amani baina ya Israil na Palestina yaanze tena.
Piya aliuomba ulimwengu uwasaidie watu wenye njaa katika Pembe ya Afrika.
Aliwaombea wanyonge walioathirika na ukame, mafuriko na vita katika sehemu mbali-mbali za dunia.
Papa Benedict piya amelalamika kuwa Krismasi imefanywa biashara.
Papa aliwasihi waumini dunia nzima wasibabaishwe na mapambo ya juu-juu.
Aliwasihi watafakari juu ya yule mtoto mchanga ndani ya banda huko Bethlehem, na furaha ya kweli ya ujumbe wa Krismasi.
Papa Benedict, mwenye umri wa miaka 84, alipanda jukwaa lilomchukua hadi kati ya kanisa.

No comments:

Post a Comment