Thursday, December 15, 2011

Wanajeshi wa Marekani warudi nyumbani


Wanajeshi wa Marekani warudi nyumbani

 15 Disemba, 2011 - Saa 04:42 GMT
Rais Obama akiwakaribisha Marekani wanajeshi toka Iraq
Rais wa Marekani Barack Obama maeadhimisha kumalizika kwa vita vya Iraq kwa kupongeza "mafanikio yasiyo ya kawaida" kwa vikosi vya Marekani katika mapigano ambayo yalipingwa sana.
Katika hotuba kwenye eneo la Fort Bragg huko Carolina Kaskazini, aliwapongeza wanajeshi wale waliohudumu na kufariki dunia wakiwa vitani, pamoja na jamii zao.
Wanajeshi wa Marekani wa mwisho wanatarajiwa kuondoka kabisa Iraq katika siku chache zijazo.
Wajumbe wa chama cha Republican wamekosoa mpango huo wa kuondoa wanajeshi wakielezea wasiwasi kuhusu usalama wa Iraq, lakini raia wengi wa Marekani wanaunga mkono hatau hiyo.
Katika hotuba ya Jumatano, Rais Obama - ambaye kwa kiasi fulani alifanikiwa kuwa rais kwa msimamo wake wa kupinga vita vya Iraq - alipongeza ujasiri wa majeshi ya Marekani katika muda wa miaka takriban tisa kweney vita hivyo.

No comments:

Post a Comment