Wednesday, December 14, 2011

Huyu ndiye mwanamke mfupi duniani


BRIDGETTE Jordan, 22, ameingia kwenye Kitabu cha Rekodi za Dunia cha Guinness ambacho kitatoka mwakani, baada ya vipimo kuthibitisha kwamba ndiye mwanamke mfupi kuliko wote duniani.

Mdada huyo, amepimwa na kubainika kuwa na urefu wa sentimita 69 (futi 2).
Hata hivyo, imeelezwa kuwa Bridgette, raia wa Marekani, ni mwanamke anayejiamini licha ya umbo lake dogo.

Bridgette, anaishi Mji wa Sandoval na ni mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Kaskaskia.
Hata kaka yake Brad, 20, ni mfupi na anatajwa kuwa na urefu wa sentimita 97 (futi 3).

Bridgette, amevunja rekodi ya ya mwanamke kutoka Uturuki, Elif Kocaman, aliyekuwa na urefu wa sentimita 71 (futi 2.3

No comments:

Post a Comment