Saturday, December 3, 2011

Mr Ebbo afariki

Mr Ebbo afariki  Send to a friend
Friday, 02 December 2011 21:06
0digg
Moses Mashalla, Arusha na Vicky Kimaro
"MI MASAI bwana...nasema mi mmasai... heri Simba ile mimi kuliko samaki jamani.." Hayo ni baadhi ya maneno yaliyopo kwenye wimbo wa 'Mi Mmasai' ulioimbwa na Abel Motika maarufu kama 'Mr Ebbo' aliyefariki juzi saa tano usiku.
Mr Ebbo alifariki wakati akiendelea kupata matibabu kwenye hospitali ya Mission ya USA River jijini Arusha, ambako alikuwa amelazwa akisumbuliwa na tatizo la upungufu wa damu.
Akizungumza jana nyumbani kwao Moshono, kaka wa marehemu Moshilaa Motika alisema alipata taarifa za kifo cha mdogo wake kutoka kwa watu waliokuwa wakimuangalia wakati amelazwa.Alisema marehemu aliyezaliwa Mei 26, mwaka 1974 atazikwa kwenye makaburi ya familia yaliyopo Kijenge Mwanama, Jumatatu ijayo nyumbani kwao Moshono jijini Arusha.
Motika alisema kifo cha mdogo wake kimeacha pigo kubwa ndani ya familia yao na hapa nchini kwa jumla kutokana na mchango wake katika sekta ya muziki.Mwanamuziki mkongwe, Fredy Maliki maarufu 'Mkoloni' alisema, Mr Ebbo amesikitishwa na kifo cha msanii huyo na kusema ni pigo kubwa.
Alisema marehemu Mr Ebbo ambaye atakumbukwa na wapenzi wake wa muziki ndani na nje ya nchi kutokana na aina ya uimbaji wake ameacha watoto wawili wa kike.
Mr Ebbo  pamoja na kuwa msanii pia alikuwa mtayarishaji muziki na mmiliki wa studio ya Motika Records iliyopo jijini Tanga.
Staili yake ya kuimba katika lugha ya Kimasai kulimfanya kujizolea umaarufu mkubwa ndani na nje ya nchi.
Baadhi ya nyimbo zake zilizowahi kutamba ni pamoja na ile ya 'Mi Mmasai', 'Mbando', 'Kamongo' na 'Maneno Mbofu Mbofu'. Marehemu ameacha mke na watoto watatu.

No comments:

Post a Comment