Saturday, December 24, 2011

Djibouti yatuma wanajeshi Somalia


Maandamano mengine yafanywa Urusi

 24 Disemba, 2011 - Saa 13:21 GMT
Maandamano mengine yanafanywa Urusi kupinga matokeo rasmi ya uchaguzi wa bunge uliofanywa awali mwezi huu.
Biramu dhidi ya Putin kwenye maandamano
Waliopanga maandamano wanadai kuwa uchaguzi huo urejelewe, kwa sababu wanasema kulitokea udanganyifu.
Makundi ya watu yamekuwa yakikusanyika katikati ya Moscow, katika maandamano ambayo yanatarajiwa kuwa makubwa.
Huko Vladivostok, mashariki mwa Urusi, waandamanaji walibeba mabiramu kutaka waziri mkuu, Vladimir Putin, afikishwe mahakamani.
Chama cha Bwana Putin kilishinda uchaguzi huo, lakini kura kilizopata zilikuwa kidogo kushinda uchaguzi wa kabla.
 

Djibouti yatuma wanajeshi Somalia

 24 Disemba, 2011 - Saa 14:16 GMT
Wanajeshi 100 wa Djibouti wamewasili Somalia kulipa nguvu jeshi la Umoja wa Afrika linalopambana na wapiganaji wa Kiislamu.
Mogadisu
Wanajeshi hao wamejumuika na wanajeshi wa Uganda na Burundi ambao tayari wako mji mkuu, Mogadishu.
Uchina imeupa Umoja wa Afrika zaidi ya dola milioni-nne kununua vifaa.
Wakati huo-huo wapiganaji wa Kiislamu wa al-Shabaab wamekuwa wakiajiri na kuwapa mafunzo wapiganaji zaidi, katika maeneo wanayodhibti nchini Somalia.

No comments:

Post a Comment