Friday, December 9, 2011

Mkutano wa hali ya hewa wapungua umuhimu

Mkutano wa hali ya hewa wapungua umuhimu

 8 Disemba, 2011 - Saa 14:16 GMT
Mkutano wa hali ya hewa wakosa umuhimu Durban
Kupungua kwa umuhimu katika kumbi za mikutano na masuala yenye msukumo kutoka maeneo mengine vinatishia kuzuia kupiga hatua katika kilele cha mkutano wa mabadiliko ya hali ya hewa unaoelekea kumalizika.
Baadhi ya washiriki wamesema hakuna hatua madhubuti za kumaliza mgawanyiko.
Wengine wanashauri kuwa mkutano wa Muungano wa Ulaya Alhamis na Ijumaa ulitakiwa unawafanya viongozi wa Ulaya wafikirie zaidi mzozo wa sarafu ya Euro na sio mgogoro wa hali ya hewa.
Mataifa mengi yanaonekana kutaka makubaliano thabiti lakini kuna kasoro kutoka kwa mataifa yenye nguvu zaidi.
Marekani, India, China na Brazil ni miongoni mwa nchi zinazoelekea kupinga baadhi ya vipengele vinavyotaka suluhisho la Muungano wa Ulaya na mataifa makubwa yanayoendelea.
Wakati mataifa hayo manne kwa pamoja yanachangia kwa zaidi ya nusu ya uharibifu wa mazingira duniani, lugha ya kidiplomasia inakuwa ngumu kuliko tarakimu zinavyoonyesha.
Zikiwa zimebaki siku mjini Durban, baadhi ya washiriki wenye uzoefu walisema mazungumzo zinaonyesha kukosa umuhimu.
Kwa hatua hii mkutano wa mwaka jana wanasema waandalizi wa Mexico walikuwa tayari wameamua hatua ya kutatua tofauti zilizojitokeza, lakini hili halijajitokeza Afrika Kusini.
Hatua za mwisho za majadiliano mara nyingi zinahusu wito kadhaa kutoka kwa wakuu wa nchi ambao wakati mwingine wanavunja ukimya kwenye maeneo ambayo wawakilishi wao hawawezi.
Lakini kukiwa na mataifa ya Muungano wa Ulaya yakitafuta suluhu ya mzozo wa sarafu ya Euro katika mkutano wao wa Brussels, washiriki wanahoji iwapo viongozi wa Ulaya wana muda wa kutoa wito muhimu.

No comments:

Post a Comment