Ujumbe wa Kiarabu wawasili Syria
26 Disemba, 2011 - Saa 10:02 GMT
Uumbe wa wachunguzi kutoka
Jumuia ya Nchi za Kiarabu unatarajiwa nchini Syria leo, kuanza
kuchunguza kazi ya kumaliza ghasia ambazo Umoja wa Mataifa unasema,
zimesababisha vifo vya watu zaidi ya 5000 tangu mwezi wa March.
Ujumbe wa kwanza wa nchi za Kiarabu uliwasili Damascus juma lilopita.
Sasa maafisa wengine 50 watajumuika nao leo.
Kufuatana na makubaliano wajumbe hao watakuwa na uhuru wa kuzuru watakako kuona yanayotokea.
Umoja wa upinzani, Halmashauri ya Taifa ya Syria, imewasihi wajumbe hao kwanza kuzuru mji wa tatu kwa ukubwa, Homs.
Upinzani unasema mtaa mmoja wa mji huo, Baba Amro, umezingirwa na askari wa usalama na unashambuliwa kwa mabomu, na kwamba watu wengi wamekufa.
Syria imesema imechukua dhamana ya kuwalinda wajumbe hao, kwa hivo haijulikani kama watakuwa na uhuru kamili wa kuzuru maeneo ya ghasia.
Mkuu wa Jumuia ya Nchi za Kiarabu, Nabil al-Arabi, amesema itachukua kama juma moja kuamua kama Syria inafuata mkataba iliyotia saini; ambao unataka wajumbe hao wahakikishe kuwa Syria imeacha kutumia nguvu, imeondoa wanajeshi na kuwaachilia huru wafungwa, ambao inasemekana ni maelfu.
No comments:
Post a Comment