Friday, January 13, 2012

Wizara: Ugawaji vitalu vya uwindaji haurudiwi


 Send to a friend
Friday, 13 January 2012 10:13
0digg
Twiga wakiwa katika hifadhi ya mlima KIlimanjaro
Boniface Meena
WIZARA ya Maliasili na Utalii imesema haina mpango wa kurudia ugawaji wa vitalu vya uwindaji kwa kuwa mchakato wa ugawaji ulikamilika Septemba mwaka jana na matokeo yake kutangazwa wazi.

Taarifa ya wizara hiyo iliyosaniwa na  msemaji wake, George Matiko, ilisema mapema Septemba mwaka jana, wizara ilitoa orodha ya kampuni 60 zilizofanikiwa kugawiwa vitalu na kwamba kampuni 51 miongoni mwa hiozo ni za kizalendo na tisa nyingine ni za kigeni.

Taarifa hiyo ilisema ufafanuzi huo unafuatia  taarifa zinazoripotiwa na baadhi ya vyombo vya habari zikiashiria harakati za  waombaji waliokosa vitalu,  kuchafuana na wae waliopata.

"Wizara inasisitiza kuwa mchakato wa ugawaji wa vitalu hautarudiwa na Watanzania wanahakikishiwa kuwa hatua zilizochukuliwa na Serikali za kuleta mabadiliko kwenye sekta hii tangu mwaka 2008, zimesaidia sana kuimarisha usimamizi wa sekta," ilisema taarifa ya Matiko. "Kuna mabadiliko zaidi ya 21 yaliyofanyika tangu wakati huo kwa kuzingatia sheria ya wanyamapori na hivyo haitakuwa rahisi kwa mtu au kikundi cha watu kufanya tofauti," ilisisitiza taarifa.
Alisema wizara imesikitishwa na taarifa zilizoripotiwa na gazeti moja la kila siku(siyo Mwananchi) likinukuu taarifa kutoka Dallas, Marekani kwamba ugawaji wa vitalu utarudiwa kwa shinikizo la Ikulu.
"Madai hayo siyo kweli na  wizara haijapokea maelekezo yoyote kutoka Ikulu wala sehemu nyingine yoyote kuhusu suala hili la vitalu,"alisema Matiko.

Alisema wizara inasisitiza kuwa waombaji waliopata vitalu wamehakikiwa na waziri na kuwa barua walizopokea kutoka wizarani kuhusu kugawiwa vitalu ni nyaraka halali za wizara.

No comments:

Post a Comment