Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo linadai kuwa wapiganaji kutoka Rwanda waliwaua raia 26 mashariki mwa nchi hiyo.
Jeshi hilo la Congo limesema mashambulio hayo yalitekelezwa na waasi wa kundi la FDLR, mapema wiki hii.Mauaji hayo yanawakilisha baadhi ya mapigano makali zaidi kutekelezwa na kundi hilo kwa miezi sasa.
Jeshi la Congo limesema litaimarisha ulinzi katika eneo hilo.
Miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa ni Bamuguma Sid, mkoa wa kivu ya kusini.
Mbali na kuwauwa watu, wapiganaji wa FDLR inadaiwa kupora mali wakaazi wa eneo hilo.
Walionusurika shambulio hilo wameripotiwa wakisema kuwa walilengwa kwa sababu jamii kutoka eneo hilo linadhaniwa kuunga mkono kundi la wanamgambo katika eneo hilo, na kwamba walikuwa wanaadhibiwa kwa hilo.
Wapiganaji wa FDLR wamelaumiwa kwa kutekeleza ubakaji na mauaji , licha ya kuwepo kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa katika eneo hilo.
No comments:
Post a Comment