Nahodha wa meli iliyopinduka alaumiwa
17 Januari, 2012 - Saa 04:13 GMT
Idadi ya watu wasiojulikana
walipo baada ya meli ya kifahari kupinduka katika ufuo wa Italia Ijumaa
iliyopita, imefikia watu 29, watu sita kati yao wakiwa wamethibitishwa
kufariki.
Wakati shughuli za uwokozi zikiendelea, shirika
la habari la Italia (Ansa), limeripoti kuwa nahodha wa meli hiyo
Francesco Schettino, amelaumiwa kwa kukwepa juhudi za kuwaokoa waliokuwa
wakizama katika meli hiyo.Nahodha huyo anayehojiwa na maafisa wa polisi, pia amelaumiwa na mwenye meli kwa kuacha makusudi kufuata njia ya kawaida ya meli hiyo.
Hata hivyo nahodha huyo anasisitiza kuwa alifuata utaratibu sawa wakati wote alipokuwa katika meli hiyo.
nahodha akamatwa
Nahodha wa meli hiyo amekamtwa kwa tuhuma za mauaji na jaji anatarajiwa baadaye hii leo kuamua iwapo nahodha huyo mweye umri wa miaka 52 ataendelea kushikiliwa na polisi .Italia imesema itatangaza hali ya tahadhari kufuatia kupinduka kwa meli hilo, na kwamba itatoa msaada kuzuia janga lolote kwa mazingira.
Waziri wa mazingira wa Italia anasema anahofia kuwa mafuta huenda yakavuja kutoka kwenye meli hiyo.
Watu ambao bado hawajapatikana ni pamoja na wafanyikazi wa meli hiyo pamoja na abiria kutoka Marekani, Ufaransa na Italia.
No comments:
Post a Comment