Watu 40 watoweka katika ajali ya meli
14 Januari, 2012 - Saa 20:10 GMT
Wakuu wa forodha wa Utaliana
wanasema watu kama 40 bado wametoweka, baada ya meli ya abiria iliyobeba
watu zaidi ya 4000 kwenda mrama katika mwambao wa Utaliana.
Msemaji wa walinzi wa pwani alieleza inawezekana kuwa watu wengine bado wako ndani ya meli.
Abiria wawili kutoka Ufaransa na baharia mmoja kutoka Peru wanajulikana kuwa wamekufa.
Mkuu wa kampuni inayomiliki meli hiyo, Gianni Onorato, alisema ushahidi wa awali unaonesha kuwa meli iligonga mwamba;
nahodha haraka akafuata utaratibu wa kuwatoa abiria melini.
Lakini operesheni ilizuwilika kwa sababu meli yenyewe haraka ilipindukia ubavuni na kuzusha mtafaruku.
Taarifa za karibuni zinaeleza kuwa ofisi ya mashtaka ilimzuwia nahodha baada ya kumhoji.
No comments:
Post a Comment