'Boko Haram wanamizizi serikalini'
9 Januari, 2012 - Saa 04:56 GMT
Rais wa Nigeria Goodluck
Jonathan kwa mara ya kwanza amesema anahofia kuwa kundi hilo la waislamu
wenye msimamo mkali wanaungwa mkono na baadhi ya maafisa wa usalama na
wakuu wa serikali.
Kiongozi huyo amesema hali ya usalama nchini humo sasa ni mbaya na ya kutatiza kuliko wakati wa vita vya wenyewe kwa wenye vilivyoshuhudiwa nchini humo kati ya mwaka wa 67 na 70.
Wakati wa vita hivyo zaidi ya watu milioni moja waliuawa.
Mamia ya watu hasaa wakristo wamelazimika kuhama mkaazi yao kufuatia mashambulio yaliodumu saa 24 wiki iliopita yaliotekelezwa na makundi ya watu wanaoaminika kuwa ni wafuasi wa Boko Haram.
Kundi hilo la Boko Haram lina lengo la kuipindua serikali na kuteua utawala wa kiislamu nchini Nigeria.
Akizungumza wakati wa Ibada katika kanisa la Rememberance Day mjini Abuja, Rais Jonathan alisema usalama nchini humo upo katika hali mbaya sana kwa kuwa imekuwa vigumu kumtambua adui.
"wengine wapo serikali, kwenye jeshi, polisi na hata kwenye idara ya mahakama, hali ni mbaya sana, ata ikiwa mtoto wako ni mwanachama wa kundi hilo hauwezi kujua" alisema kiongozi huyo.
Viongozi wa kikristo wanailaumu serikali kwa kutowalinda dhidi ya mashambulio hayo yanayowalenga.
Wiki iliopita Rais Jonathan alitangaza hali ya hatari katika majimbo ya Yobe, Borno, Plateau na Niger kufuatia mashambulizi hayo.
No comments:
Post a Comment