Tuesday, January 3, 2012

Mafuta yapanda bei sana Nigeria 2 Januari, 2012 - Saa 14:07 GMT

Mafuta yapanda bei sana Nigeria

 2 Januari, 2012 - Saa 14:07 GMT
Bei ya mafuta nchini Nigeria imepanda zaidi ya mara dufu baada ya serikali kuamua kuacha kufidia bei ya mafuta.
Wachuuzi wa petroli nchini Nigeria
Vyama vya wafanyakazi vimetoa wito kwa watu kujitayarisha kwa migomo na maandamano.
Serikali inadai kuwa kuondosha fidia hiyo inayoigharimu dola bilioni 6 kila mwaka, inamaanisha kuwa itakuwa na fedha kutumia kwenye miradi ya kupunguza umaskini.
Lakini Wanigeria wengi hawaamini kuwa wataona manufaa yoyote katika hatua za kupunguza ufukara.
Mwanaharakati wa wafanyakazi, John Odah, aliiambia BBC kwamba Nigeria haifai kuagizia petroli kutoka nchi za nje, na serikali inafaa kushughulikia kujenga mitambo ya kusafisha mafuta nchini.
"Nafikiri serikali haikuweza kujibu hoja kwamba nchi inayotoa mafuta kama sisi, haifai kuagiza petroli kutoka nje.
Kwa hivo serikali inafaa kuupa umbele mradi wa kuwa na vinu vya kutosha vya kusafisha mafuta nchini mwetu.
Lakini hatuoni kuwa serikali inaelekea huko."

No comments:

Post a Comment