Tuesday, January 3, 2012

Iran yajaribu makombora zaidi BAHARI YA HORMUZ


Iran yajaribu makombora zaidi

 2 Januari, 2012 - Saa 17:12 GMT
Iran inasema imefanikiwa katika majaribio ya makombora mawili zaidi, na inaonekana inataka kuonesha nguvu zake za kijeshi, siku ya mwisho ya mazoezi ya jeshi lake la wanamaji karibu na mlango wa bahari wa Hormuz.
Manuwari ya Iran ikifyatua kombora karibu na Hormuz
Kamanda wa jeshi la wanamaji la Iran, Mahmoud Mousavi, alisema kombora la kushambulia meli, lilotengenezwa Iran, liliipiga lengo; na kombora aina nyengine lilojaribiwa lilikuwa bora zaidi kushinda la awali.
Mwandishi wa BBC anasema Iran inataka kuonesha kuwa inaweza kudhibiti njia ya bahari ya Hormuz, ambapo ndipo meli nyingi zinazosafirisha mafuta zinapopita.
Anasema inatoa ujumbe kwa Mataifa ay Magharibi kwamba inaweza kutengeneza makombora yake yenyewe, juu ya kuwa imewekewa vikwazo kwa sababu ya mradi wake wa nuklia.

No comments:

Post a Comment