Sunday, January 8, 2012

Al-Bashir aishukuru Libya

Al-Bashir aishukuru Libya

 8 Januari, 2012 - Saa 16:33 GMT
Rais Omar al-Bashir, ambaye anazuru Libya, amesema anaweza kuisaidia Libya kuwafanya wapiganaji wa zamani kusalimisha silaha na kuwajumuisha kwenye jeshi na polisi.
Rais al-Bashir akizuru Libya
Wapiganaji wanaopingana nchini Libya wanashindana kuhodhi madaraka baada ya kuondoshwa kwa Kanali Gaddafi.
Rais al-Bashir aliwaambia wenyeji wake kwamba ana uzoefu wa kuwaleta pamoja wapiganaji.
Rais al-Bashir, akiwa pamoja na wakuu wa Libya, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Sudan inaishukuru Libya kwa kuiunga mkono Sudan:
"Tumekuja kuwashukuru ndugu zetu wa Libya na wapiganaji wa Libya kwa yale waliyotufanyia sisi nchini Sudan.
Kwa kuishinda serikali ya Gaddafi, wametupa zawadi kubwa kabisa katika historia yetu ya sasa."
Kiongozi wa serikali ya muda ya Libya, Mustafa Abdel-Jalil alisema nchi zao zitazidisha ushirikiano katika usalama.
Hata hivo, mashirika ya kutetea haki za kibinadamu yanasema kwa vile Rais al-Bashir anasakwa kwa uhalifu aliofanya vitani, ziara yake nchini Libya inakwenda kinyume na ahadi ya Libya kwamba inataka kuendeleza demokrasi na nidhamu.
Serikali ya Kanali Gaddafi ikiwasaidia wapiganaji wa Darfur.

No comments:

Post a Comment