Polisi wanasa shehena ya Heroin Lindi | Send to a friend |
Saturday, 14 January 2012 08:53 |
0digg
Bernard JamesKIKOSI cha Polisi cha Kupambana na Dawa za Kulevya mkoani Lindi, kimekamata kilo 210 za Heroine, kiasi ambacho ni kikubwa kukamatwa tangu kuanzishwa kikosi hicho mwaka1990.Kukamatwa kwa dawa hizo juzi, kulikuja baada ya polisi kuvamia nyumba ya mkazi wa Mchinga II na kukuta kiasi hicho. Mkuu wa Kikosi cha Polisi cha Kuzuia Dawa za Kulevya Nchini, Godfrey Nzowa, alithibitishia habari hizo juzi kwa njia ya simu.Alisema katika nyumba hizo, polisi walikutana watu watatu wakijiandaa kusafirisha dawa hizo kwenda jijini Dar es Salaam. “Baada ya kupoka taarifa kutoka kwa msiri wetu nilituma vijana wa kikosi chetu cha ambao kwa kushirikiana vyema na wenzao wa Lindi, walifanikisha kuwakamata watuhumiwa,” alisema Nzowa.Alisema kiasi cha dawa zilizokamatwa ni kikubwa kuwahi kutokea tangu kitengo chake kilipoanzishwa miongo miwili iliyopita. Nzowa alisema wafanyabiashara wa dawa hizo ambao awali walipendelea zaidi kupitia Bandari za Tanga na Bagamoyo sasa wameamua kuingilia Bandari za Lindi na Mtwara. Alisema hali hiyo inatokana na kuimarishwa kwa shughuli za ukaguzi katika Bandari ya Tanga na maeneo ya Bagamoyo. Kukamatwa kwa shehena hiyo, kumekuja miezi kadhaa baada ya Umoja wa Mataifa kuonya kuwa Afrika Masharikil imekuwa ikipokea kiasi kikubwa cha Heroine kutoka Afghanistan na Iran na kwamba hiyo inatokana na ukanda kuwa njia rahisi ya kusafirishia dawa hizo kwenda Ulaya, Amerika Kaskazini na sehemu nyingine za dunia. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wafanyabiashara wa dawa za kulevya wanatumia vizuri uwezo mdogo wa kiulinzi katika bandari and viwanja vya ndege kushamirisha biashara yao. |
No comments:
Post a Comment