Afisa wa meli aokolewa Utaliana
15 Januari, 2012 - Saa 14:15 GMT
Waokozi katika meli iliyokwenda
mrama huko Utaliana, wamemnusuru abiria mwengine, ambaye ni mmoja kati
ya maafisa wa meli hiyo, Costa Concordia.
Aliokolewa saa 36 baada ya meli hiyo, Costa Concordia, kupanda mwamba karibu na kisiwa cha Giglio, kwenye mwambao wa magharibi wa Utaliana.
Jana usiku watu wawili kutoka Korea Kusini, waliokuwa kwenye fungate, walinusuriwa
Inajulikana kuwa watu watatu wamekufa, lakini wengi bado wametoweka.
Nahodha wa meli amekamatwa.
Cosimo Nicastro wa kikosi cha walinzi wa pwani wa Utaliana, aliielezea BBC kwamba shughuli za uokozi ni ngumu:
"Ni kazi ngumu na ya hatari, kwa sababu meli yenyewe haikutulia kabisa.
Sehemu ya meli iko ndani ya maji.
Na usiku ni shida zaidi na hatar
No comments:
Post a Comment