Wasunni Iraq waacha kususia bunge
29 Januari, 2012 - Saa 17:13 GMT
Chama kikuu cha Wasunni nchini
Iraq kinasema kitaacha kususia bunge, ili kusaidia kupunguza msukosuko
wa kisiasa, ambao watu wengi wakiona unaweza kurejesha vita vya kidini.
Lakini chama hicho kimesema kwa sasa, kitaendelea kususia baraza la mawaziri.
Msukosuko ulizuka mwezi uliopita baada ya waziri mkuu, Nouri al-Maliki, ambaye ni Shia, kutoa amri kuwa kiongozi mmoja wa Iraqiya akamatwe.
Wanasiasa wa Kisunni walimuelezea Bwana Maliki kuwa dikteta.
Mashambulio kadha ya mabomu dhidi ya maeneo ya Washia yalizidisha wasiwasi.
No comments:
Post a Comment