Sunday, January 29, 2012

Viongozi wa AU wakutana


Viongozi wa AU wakutana

 29 Januari, 2012 - Saa 16:26 GMT

Mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika umeanza mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Makao Makuu mepya ya AU, mjini Addis Ababa
Kumetolewa wito kuwa nchi mbili za Sudan zimalize mizozo yao kuhusu mafuta, ambayo wadadisi wanasema, inatishia kuzusha tena vita kamili.
Na katika hotuba yake, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, ametoa wito kwa viongozi wa Sudan kufikia makubaliano.
Huu ndio mkutano wa mwanzo wa kilele wa AU tangu maandamano ya nchi za Kiarabu kuanza, na kumetolewa onyo kwamba ikiwa uongozi haikutengenea, basi mtibuko huo unaweza kutapakaa hadi kusini.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, alisema matukio yameonesha kuwa ukandamizaji siyo suluhu.
Alisema wanaume na wanawake walioandamana mitaani walitia moyo, na waliwakumbusha viongozi kwamba lazima wawasikilize.
Mkutano huu unaofanywa kwenye jengo jipya la AU, lilojengwa kwa msaada wa Uchina, unatokea wakati kuna wasiwasi mkubwa kuhusu mvutano baina ya Sudan Kaskazini na Kusini.
Baadhi ya wadadisi wanaonya kuwa vita kamili vinaweza kuanza tena baina ya majirani hao wawili.

No comments:

Post a Comment