Wednesday, January 11, 2012

Romney atwaa ushindi New Hampshire- USA

Romney atwaa ushindi New Hampshire

 11 Januari, 2012 - Saa 03:23 GMT
Mitt Romney amepiga hatua moja kubwa ya kupata tiketi ya chama cha Republican baada ya kupata ushindi katika jimbo la New Hampshire.
Mitt Romney
Romney amepiga hatua kupata tiketi ya Republican
Kufikia sasa kura bado zinahesabiwa lakini katika asilimia 19 ya vituo vya kura, Romney alikuwa anaongoza wenzake na asimia 35 ya kura zilizopigwa.
Dakika 20 baada ya vituo kufungwa Romney alihotubia wafuasi wake na kutangaza ushindi wake.
Mbunge wa Congress kutoka jimbo la Texas, Ron paul ndiye wa pili kwenye kura hizo akiwa na asilimia 25 na nafasi ya tatu imechukuliwa na John Huntsman, aliyekuwa gavana wa jimbo la Utah akiwa na asilimia 17.
Katika hotuba yake Romney ambaye alikuwa gavana wa zamani wa jimbo la Massachusetts, alikashifu sera za Rais Barack Obama za kiuchumi akisema kuwa mikakati ya kisosholisti ya ulaya kamwe haiwezi kuokoa jahazi la marekani.
"Rais Obama hana mipango na muda wake tayari unakwisha" alisema Romney.
Romney pia aliwashambulia wapinzani wake kwenye kinyanganyiro hicho wanaopinga sera za biashara huria.
Mwaka wa 2008, Mitt Romney aliibuka wapili katika jimbo hilo la New Hampshire ambapo alishindwa na John McCain.
Wajumbe wa chama cha Republican katika majimbo yote nchini Marekani watapiga kura kumchangua mgombea urais katika miezi ijayo na hatimae mshindi atatangazwa mwezi Agosti katika mkutano mkuu wa wajumbe wa chama hicho utakaofanyika katika jombo la Florida.

No comments:

Post a Comment