ANC yamazila sherehe za kutimiza karne
8 Januari, 2012 - Saa 15:09 GMT
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini
amehutubia maelfu ya wafuasi wa ANC, katika sherehe zinazomalizika leo
za kuadhimisha miaka 100 tangu chama hicho kuundwa - chama kikongwe
kabisa cha ukombozi barani Afrika.
Bwana Nelson Mandela hakuweza kuhudhuria kwa sababu ni dhaifu.
ANC hivi karibuni imekumbwa na kashfa za rushwa na mizozo ndani ya chama lakini bado kina wafuasi wengi
Kati ya wageni waliohudhuria sherehe hizo ni Kasisi Jesse Jackson, mwanaharakati maarufu wa Marekani wa kutetea haki za weusi.
Alisema: "Baada ya karne moja - kutoka madhalilisho, kachomoza Nelson Mandela, Thabo Mbeki, Jacob Zuma, na Barack Obama.
Ni karne ya mifano ya kuvuka vizingiti vikubwa.
Na khofu waliyokuwa nayo wazungu - kwamba weusi watalipiza kisasi - hayakutokea hayo".
No comments:
Post a Comment