Monday, November 28, 2011

Mvutano kuhusu uchafuzi wa hali ya hewa

Mvutano kuhusu uchafuzi wa hali ya hewa

 28 Novemba, 2011 - Saa 12:56 GMT
Uchafuzi wa hali ya hewa
Uchafuzi wa hali ya hewa
Wakati huu ambapo kikao cha viongozi kuhusu hali ya hewa kinaanza, baadhi ya nchi zinazostawi ulimwenguni ambazo zinahusika sana katika uchafuzi wa hewa zinajaribu kuchelewesha mazungumzo kuhusu mkataba mpya wa hali ya hewa ulimwenguni.
India na Brazil zimeungana na nchi tajiri katika kuitisha mazungumzo hayo yasifanyike kabla mwaka 2015, hili limeyaudhi sana mataifa madogo ya visiwani.
Muungano wa Ulaya na maeneo ambayo yako katika hatari ya mikasa kutokana na hali mbaya ya hewa wanataka mazungumzo hayo yaanze mara moja na azimio kukamilika kufikia mwaka 2015.
Kikao hicho cha Umoja wa Mataifa kinachofanyika Durban, Afrika Kusini huenda kitafanikiwa kupiga hatua katika masuala kadhaa.
"Sisi tuko Durban kwa sababu muhimu: kutafuta suluhisho kwa pamoja ambalo litahakikisha kuwepo na maisha bora na salama kwa vizazi vijavyo" amesema Bw Maite Nkoana-Mashabane, waziri wa uhusiano wa kimataifa wa Afrika Kusini ambaye ndiye mwenyekiti wa kikao hicho.
Lakini utaratibu wa kutafuta suluhu ya pamoja na kuafikiana kuhusu mkataba wa kukabiliana na uchafuzi wa hali ya hewa kuhakikisha kiwango cha joto duniani hakitazidi nyuzi joto kwa vipimo vya sentigradi 2,utakabiliwa na wakati mgumu .
Nchi zinazostawi bila shaka zitazilenga serikali tajiri kama Japan, Canada na Urusi kutokana na nchi hizo kukataa kujihusisha katika makubaliano mapya ya kupunguza uchafuzi chini ya mkataba wa hali ya hewa wa Kyoto ambao makubaliano yake kuhusu uchafuzi wa hewa na njia za kukabiliana nao yanamalizika mwaka ujao.
Wanaolalamika wanaona kama huu ni ukiukaji wa uwajibikaji na uaminifu.
Lakini baadhi ya wachunguzi wanasema mataifa madogo ya visiwani huenda yakayataja hadharani mataifa yanayostawi ambayo yanachelewesha utaratibu huu kwa kusudi.
Wanasema mvutano huu hupaswi kuchelewesha makubaliano mapya, ambapo mmoja wa washiriki katika mkutano amesema ikiwa hilo litafanyika basi itakuwa ni "uzingativu wa siasa za uharibifu."
Mjumbe mwengine ameiambia BBC kuwa wanaopinga "Wako ukingoni na katika hatari ya kuporomoka" aliongeza kuwa " na huenda wasiweze kujikwamua kutoka janga hilo".

No comments:

Post a Comment