Tuesday, November 29, 2011

Aota ‘shipa’ lenye kilo 45

Aota ‘shipa’ lenye kilo 45 

November 1, 2011 at 9:28am

WESLEY Warren Jr., 47 (pichani), raia wa Marekani, anaishi kwa mateso makubwa kutokana na ‘shipa’ lililomuota ambalo hivi sasa limefikisha uzito wa kilo 45.

Kutokana na shipa hilo, Warren hawezi kutembea na hata kunyanyuka sehemu aliyopo ili aende chooni ni mtihani tata.
Mtihani mkubwa kwa Warren ni matibabu, kuweza kumaliza uvimbe alionao, kwani unagharimu dola milioni 1 (shilingi bilioni 1.7).

Hata hivyo, madaktari wanasema kuwa Warren anaumwa ugonjwa wa matende ambao huambukizwa kwa kung’atwa na mbu.

Taarifa hiyo ya madaktari, Warren anaipinga kwa maelezo kuwa hajawahi kuishi mazingira ya tropiki kama Afrika na Asia ambayo huruhusu mazalia ya mbu.

Warren ambaye ni mkazi wa Las Vegas, ameshautangazia ulimwengu kuwa anahitaji msaada wa hali na mali ili apate fedha hizo zitakazomuwezesha kupata matibabu.

Tatizo alilonalo limekuwa likimsababisha kushindwa hata kuoga kwani uzito unamuelemea.
“Si rahisi hata kujizungusha,” Wisley aliliambia gazeti moja la  Las Vegas na kuongeza kuwa hali hiyo inamfanya muda mwingi awe amekaa.

Wesley alianza kuumwa ugonjwa huo miaka mitatu iliyopita na kumfanya apatwe na hali ya wasiwasi pamoja na msongo wa mawazo.

“Natamani kuwa na rafiki lakini naogopa hata kuingia katika uhusiano wa kimapenzi, kila mwanamke namhofia kwa maana sijiamini kama naweza kumpata mtu anayenipenda.

“Pamoja na yote, siwezi kusema nijiue, najipa imani na matumaini. Nina nguvu sana,” anasema Warren.
Akionekana na kusikika kwenye redio na televisheni ya Howard Stern, Warren alimwaga machozi, akiomba walimwengu wamsaidie kupata fedha za matibabu.

“Sikutaka kujidhalilisha lakini kwa sababu nilijua kuwa televisheni na redio, inatazamwa na kusikilizwa na mamilioni, natumaini watu wakishasikia shida yangu, wanaweza kunisaidia,” alisema.
Kuhusu alivyoanza kuumwa, Warren anasema kuwa alianza kusumbuliwa na miguu pamoja na korodani kabla ya kugeuka ‘shipa’ kubwa.

No comments:

Post a Comment