Tuesday, April 3, 2012

Wabunge: Tulicharangwa mapanga mbele ya polisi - Kirumba

Wabunge: Tulicharangwa mapanga mbele ya polisi  Send to a friend
Monday, 02 April 2012 21:37
0digg
Mbunge wa Ilemela, Highnes Kiwia akihudumiwa na Muuguzi Mwandamizi katika Wodi ya Kibasila,Ezelina Zambi,kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Jijini Dar es Salaam jana. Mbunge huyo na mwezake wa Ukerewe Salvatory Machemli walijeruhiwa Jijini Mwanza wakati wa uchaguzi mdogo wa Udiwani Kata ya Kirumba juzi Jumapili. Picha na Joseph Zablon
Joseph Zablon
WABUNGE wawili wa Chadema ambao walijeruhiwa kwa mapanga na mashoka katika uchaguzi mdogo wa udiwani Jimbo la Kirumba, Mwanza wamesema walipata kipigo hicho mbele ya polisi.

Wakizungumza jana katika Chumba namba 310, Wodi 16 Jengo la Kibasila, Hospitali ya Taifa Muhimbili, wabunge hao walidai kuwa walipigwa na vijana wa CCM ambao walikuwa na watu wanaowatambua huku polisi wa doria wakishuhudia.
Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia alisema kilichotokea hakukitarajia na haamini kama polisi wanaweza wakashirikiana na majambazi kujeruhi wengine.

“Nilipofika Ibanda Kabuhoro, kuna gari lilikuwa mbele yangu likasimama, wakashuka watu kama 19 hivi, wakavunja kioo cha mbele cha gari langu. Kuna polisi alikuwa amebeba silaha jirani akasogea, nilipojaribu kufungua kioo kuzungumza naye nikapuliziwa ‘spray’ ambayo siitambui,” alisema.

Kiwia alisema watu hao walikuwa wakiwashambulia huku polisi wakiangalia… “wakati wote walitaka nitoe silaha ambayo walidai kuwa ninayo huku wakinipiga na walianza kwa kunipiga na rungu jichoni na kisha nikavutwa hadi nje ya gari na kukanyagwa usoni.”

Mbunge huyo alisema watu hao waliendelea kumpiga licha ya jitihada zake za kuomba msaada kwa polisi hazikuzaa matunda na hata alipojaribu kushika suruali ya polisi ili ajinusuru kwa kipigo, hakufanikiwa na ghafla alipigwa na kitu kizito kichwani.

“Fahamu zilinivurugika, nilijikokota hadi katika gari la doria la polisi na wakati najaribu kupanda polisi mwingine mwenye bunduki begani alinibeba na kunitupa garini,” alisema Kiwia na kuongeza kwamba ndani ya gari hilo aligundua kuwa ametupwa juu ya mwili wa Mbunge mwenzake, Salvatory Machemli.

Alisema hayo yakitokea alipokuwa akielekea eneo la Magnum ambako walielezwa kuwa kuna wana CCM ambao wamejikusanya sehemu ambako aliambiwa kuwa huenda walikuwa wanagawana rushwa.

Hata hivyo, alisema alipofika Ibanda gari lililokuwa mbele yake lilisimama… “Ile barabara ni nyembamba hivyo nikawa nasubiri, ghafla wakashuka watu kama 19 na mara gari jingine likaja na kusimama nyuma ya la kwangu, hofu ikaniingia nikapiga simu kwa Wenje (Mbunge wa Nyamagana Chadema) ambaye hata hivyo, simu yake ikawa haipatikani.”
Mbunge huyo alisema alimpigia pia Machemli ambaye alipokea na kumweleza kuwa ametekwa na pia akaifahamisha pia polisi lakini, akiwa bado amezungukwa na watu hao gari la Machemli lilifika eneo la tukio na lilizingirwa na wahalifu hao ambao pia walimpatia kipigo.

“Muda mfupi baadaye polisi walifika na wawili kati yao wakiwa na silaha za moto na mmoja wao alisimama jirani na mlango wa gari langu,” alisema na kuongeza kuwa ghafla kioo cha mbele cha gari lake kilivunjwa.
Alisema kuona hivyo alishusha kioo ili azungumze na polisi aliyekuwa amesimama jirani na gari lake, wakati huo mbunge mwenzake akiendelea kunyukwa lakini mbele ya polisi huyo.

“Walinishusha wakaanza kunipiga na walianza kwa kunipiga na rungu jichoni, kisha mabapa ya mapanga, nikalimwa shoka kichwani na kudondoka chini. Waliendelea kunipiga huku wakinikanyaga,” alisema.

Muuguzi wa wodi hiyo, Ezelina Zambi alisema hali za majeruhi hao zinaendelea vizuri.
“Kiwia alipiga x-ray kifuani na kichwani na anasubiri kipimo cha MRI ili kujua kama tissue za ubongo wake zimepata athari zozote,” alisema na kuongeza kuwa kama kipimo hicho kitaonyesha hakuna tatizo huenda akaruhusiwa.

Wabunge hao wawili walishambuliwa usiku wa kuamkia juzi na watu hao wasiojulikana na baada ya tukio hilo walipelekwa katika Hospitali ya Rufaa Bugando, Mwanza kabla kusafirishwa hadi Dar es Salaam.

Kiwia na mwenzake pamoja na watu wengine kadhaa walishambuliwa na wanaodaiwa kuwa ni wafusi wa CCM, hivyo kumsababishia majeraha kichwani.

Mbali wabunge hao wengine ni waliojeruhiwa ni Ahmed Waziri ambaye anadaiwa kuwa ni kada wa UVCCM aliyekatwa kiganja chake cha mkono wa kulia, Haji Mkweda (21), Judith Madaraka (26) na Ivory Mchimba (26).

Alipoulizwa jana kuhusu madai ya wabunge hao, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Liberatus Barlow alikataa kuzungumzia tukio hilo kwa maelezo kwamba polisi bado inaendelea na uchunguzi.

“Tunafanya uchunguzi, kwa sasa hata majina haya ya majeruhi ambao niliwapa unaona hayajabainisha nani ni nani,” alisema.
 Send to a friend

No comments:

Post a Comment