Waasi wa Tuareg wapata ushindi Mali
2 Aprili, 2012 - Saa 04:10 GMT
Waasi wa Tuareg nchini Mali wamesema wameuteka mji muhimu wa Timbaktu Kaskazini mwa nchi hio.
Huku hayo yakijiri, viongozi wa kijeshi
waliofanya mapinduzi ya serikali wamesema wanarejesha utawala wa
kikatiba na taasisi za nchi hiyo.Huko kaskazini, bendera ya waasi inapaa nje ya nyumba ya gavana wa Timbaktu, hatua hii inamaanisha kuwa miji yote muhimu kaskazini mwa Mali sasa iko chini ya mikono ya waasi wa Tuareg.
Waasi hao sasa wanasema kuwa wako tayari kutangaza eneo huru ambalo wataliita Azawad. Lakini sio wao tu wanaojitangazia ushindi, kundi la wapiganaji wa kiislamu walio na lengo la utangaza utawala unaozingatia sheria za kiislamu nalo pia linajivunia ushindi huo.
Imekuwa vigumu kuelewa jinsi makundi haya mawili yatagawana mamlaka.
Na katika mji mkuu Bamako, viongozi wa mapinduzi wametangaza kuwa wataunda serikali ya mpito ambayo itaandaa uchaguzi ulio wa huru na haki.
Licha ya tangazo hilo nchi jirani huenda zisilegeze shinikizo dhidi ya waasi hao hadi watakapo tangaza ratiba yao ya kuondoka mamlakani.
Na atakae twaa uongozi nchini Mali atakua amerithi matatizo makubwa zaidi ya hali ilivyokuwa, ikiwemo suala la waasi waliojitangazia eneo lao huru.
Lakushangaza wanajeshi waliofanya mapinduzi walidai sababu yao kuu ya kuipindua serikali ya Rais Amadou Toumani Toure kwa kuwa alisihindwa kuzuia harakati za waasi wa Taureg kaskazini mwa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment