Rais wa Mali kushtakiwa kwa uhaini
4 Aprili, 2012 - Saa 09:21 GMT
Watawala wa kijeshi wanapanga
kumfungulia mashtaka ya uhaini rais waliyempindua. Kiongozi wa Mapinduzi
Kapten Amadou Sanogo amesema pamoja na mashtaka mengine, Amadou Toumani
Toure anakabiliwa na ubadhirifu wa fedha za umma.
Haya yanajiri wakati watawala wa kijeshi
wametangaza kuanza kongamano la kitaifa kujadili mustakabali wa Mali.
Nchi hiyo ambayo haina bandari imewekewa vikwazo vya kiuchumi na jamii
ya kimataifa.Waasi hao wamegawanyika makundi mawili ambapo lile la MNLA linapigania kuwepo taifa huru la Azawad. Kundi nyingine Ansar Dine lenye uhusiano na mtandao wa Al-Qaeda linataka kusalia Mali lakini chini ya sheria ya Kiisilamu.
Rais Amadou Toumani Toure alitarajiwa kuondoka madarakani baada ya kumaliza muhula wake wa pili baadaye mwezi huu.Wakati huo huo Waasi hao wa Kaskazini wameendelea kusonga hatua mbele kusini mwa Mali.
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kutoa taarifa kuhusu mzozo wa Mali baadaye Jumatano wiki hii.

No comments:
Post a Comment