ECOWAS yaiwekea vikwazo Mali
2 Aprili, 2012 - Saa 17:41 GMT
Viongozi wa Ecowas waliokutana mjini Dakar, Senegal wamesema vikwazo hivi vitasalia hadi watawala wa kijeshi kurejesha madaraka kwa raia.Aidha Ecowas inatayarisha kikosi cha amani kusaidia mzozo unaokumba Mali ambapo katika siku za karibuni,waasi wa Tuareg wameteka maeneo mengi kaskazini mwa nchi.
Viongozi wa Ecowas walikuwa wamewapa watawala wa jeshi hadi Jumatatu ya wiki hii kuondoka madarakani. Kaskazini mwa Mali waasi wa Tuareg walitumia msukosuko wa kisiasa ulioko kuliteka eneo nzima la kaskazini.Waandishi wa habari wamesema Mali ambayo haina bandari itakuwa na wakati mgumu kujikimu kiuchumi kutokana na vikwazo vya sasa.
No comments:
Post a Comment