Wednesday, April 4, 2012

ANC yamfungia Malema kuwaongoza vijana


ANC yamfungia Malema kuwaongoza vijana

 4 Aprili, 2012 - Saa 18:21 GMT
Chama tawala nchini Afrika kusini, kimemtimua rais wa tawi la chama hicho la vijana,Julius Malema kutoka wadhifa wake katika chama hicho mara moja.
Kamati ya nidhamu ya chama hicho, pia imempiga marufuku Malema kuhudhuria mikutano ya chama hicho baada ya Malema kusema utawala wa rais Jacob Zuma, ni wa kidikteta.
Bwana Malema alitimuliwa kutoka ANC tangu mwezi Februari mwaka huu, lakini hadi leo aliendelea kushikilia wadhifa wa rais wa mrengo wa vijana na kuruhusiwa kuhudhuria mikutano, akisubiri kusikizwa kwa kesi yake ya rufaa baadaye mwezi huu.

No comments:

Post a Comment