Tuesday, April 3, 2012

Syria ina hadi Aprili 10 kuweka amani


Syria ina hadi Aprili 10 kuweka amani

 2 Aprili, 2012 - Saa 18:49 GMT
Mapigano yameendelea mjini Homs
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa na Muungano wa nchi za kiarabu Koffi Annan amelitaka Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuweka Aprili 10 kama siku ya mwisho kwa Syria kutekeleza mpango wake wa amani.
Kwenye kikao cha faragha kwa Baraza hilo, Bw Annan alisema sharti mapigano yasitishwe katika saa 48 baada ya siku hiyo.
Balozi wa Syria katika Umoja wa Mataifa amethibitisha kwamba serikali yake imeridhia kutekeleza mpango huo kabla ya siku ya mwisho.Aidha balozi huyo Bashar Al Jaafari amesema sharti upinzani pia umalize mashambulizi yote.
Mapigano yameendelea nchini Syria licha ya ahadi ya Rais Bashar al Assad kuitikia mpango wa amani uliopendekezwa na Koffi Annan wiki moja iliyopita.Wakati huo huo Mkuu wa Shirika la Msalaba Mwekundu ,Jakob Kellenberger anafanya ziara nchini Syria kutaka wapewe idhini ya kuwahudumia wafungwa na kusambaza misaada ya dharura.
Taarifa ya shirika hilo imesema Bw Kellenberger atajaribu kuomba kusitishwa mapigano kwa saa mbili kila siku ili kuwaondoa majeruhi na kutoa misaada ya kibinadamu.

No comments:

Post a Comment