HABARI ZA VITUKO
MFUNGWA AVAA GAUNI KUTOROKA
Viatu virefu sio jambo la mchezo
Mfungwa mmoja wa kiume nchini
Brazil aliyekuwa akijaribu kutoroka gerezani kwa kuvaa nguo za kike
amekamatwa tena na kurejeshwa ndani.
Bwana huyo Ronaldo Silva alinyoa nywele zake za
mikononi na miguuni na kutoka kupitia lango kuu la gereza akiwa amevaa
gauni la bluu, wigi kicwhani na viatu virefu.
Hata hivyo bwana huyo ambaye amefungwa kwa
makosa ya uuzaji dawa za kulevya, alishtukiwa na polisi mmoja aliyeona
akitembea tofauti na wanawake wengine mitaani.
Polisi wamesema nguo hizo aliletewa gerezani na
mke wake. Mbali na kuvalia gauni hilo na viatu virefu Ronaldo pia
alikuwa amepaka rangi ya mdomo-- lipstik nyekundu iliyokolea.
Polisi walimkamata dakika thelathini tu baada ya
kufanikiwa kutoroka gerezani kutokana na kushindwa kutembea vyema na
high heels. Mkurugenzi wa gereza hilo Carlos Welber amesema mke wake
amekiri kumletea mume wake nguo za kike, lakini amesema hakufahamu kwa
nini mume huyo alizitaka.
Mfungwa huyo alikuwa ndio kwanza tu amehamishiwa
katika gereza hilo, baada ya kufanya jaribio la kutoroka katika gereza
alilofungiwa awali.
MNYONYESHAJI ASIYEJULIKANA
Mama kwa mshangao...
Mama mmoja nchini Marekani alipatwa na mshituko
baada ya kukuta mtoto wake mchanga akinyonyeshwa ndani ya nyumba yake na
mwanamke asiyemfahamu.
Kituo cha radio cha KJJQ cha South Dakota
kimesema mama huyo alipatwa na mshangao huo saa kumi na moja alfajiri
alipokuta kichanga chake cha miezi miwili kikinyonyeshwa na mwanamama
asiyefahamika.
Mama huyo alipiga simu mara moja polisi kuripoti suala hilo.
Aidha mama huyo alimchukua mwanaye, lakini
mwanamama aliyekuwa akimyonyesha aliendelea kubaki ndani ya nyumba hiyo,
hadi polisi walipowasili na kumkamata.
Jitihada za waandishi wa habari kutafa kufahamu
zaidi kilichotokea ziligonga mwamba baada ya polisi wa kituo cha
Brookings kutopokea simu, umeripoti mtandao wa Huffington Post.
Hata
hivyo taarifa zinasema mwanamke mwenye umri wa miaka ishirini na nne
ameshtakiwa kwa kosa la kuingia katika nyumba isiyo yake kinyume cha
sheria. Pia majina ya wakinamama hao na hata kichanga hayakuweza
kupatikana mara moja.
MLEGEZO WAMPELEKA JELA
Mlegezo wampeleka jela siku tatu
Kijana mmoja mwenye umri wa miaka ishirni nchini
Marekani amehukumiwa kwenda jela kwa siku tatu kwa kuvaa suruali yake
chini ya kiuno, yaani mlegezo.
Jaji katika mahakama mjini Alabama alitoa adhabu
hiyo kwa kijana aliyekuwa amevaa suruali aina ya jeans kwa misingi ya
kukiuka maadili ya mahakama.
Kijana huyo LaMarcus D Ramsey alikuwa
amefikishwa katika mahakama ya Autagua kwa kosa la kufanya wizi,
limeripoti gazeti la Montgomery Advertiser.
Taarifa zinasema wakati kesi yake ikisikilizwa
jaji John Bush alionekana kutatizwa sana na jinsi kijana huyo alivyokuwa
amevaa suruali yake, na mara moja alitoa ari kijana huyo kupelekwa jela
kwa siku tatu kwa kosa la kuvaa suruali mlegezo, au sag.
"Unadhalilisha mahakama kwa kuonesha makalio
yako" amesema jaji huyo. Hali kadhalika jaji huyo amesema mbali na kukaa
jela kwa siku tatu, akitoka, kijana huyo ametakiwa kununua suruali
inayomtosha, au anunue mkanda, ili nguo yake ya ndani na makalio yake
visionekane.
MFUNGWA AMN'GATA AFISA MAGEREZA
Kasheshe gerezani
Mfungwa mmoja wa kike nchini Marekani
anakabiliwa na mashtaka zaidi, baada ya kumngata afisa wa magereza, siku
ya jumatatu hadi meno yake mawili kun'gooka.
Mfungwa huyo Erin Babich, alikuwa akitumikia
kifungo katika gereza la Manatee, karibu kilomita hamsini kusini mwa
Tampa, Florida. Mtandao wa Big Pond News umesema mtafaruku ulianza baada
ya Bi Babich kugoma kusikiliza mari za gereza na kujaribu kumpiga afisa
mmoja wa gereza.
Wakati akifanya fujo hizo, maafisa wengine wa
magereza walijitokeza kusadia, na ndipo alipoamua kumgnata mmoja wao
mkononi kwa nguvu mno kiasi kwamba meno yake mawili yalingooka.
Bi Babich sasa ameshtakiwa kwa kosa la
kumshambulia afisa wa magereza. Afisa aliyengatwa anapatiwa matibabu
katika hospitali ya mji huo.
POLISI ASIYEJUA KUTUMIA BUNDUKI
Shabaha sifuri
Mkuu wa Polisi wa mji mmoja nchini Marekani amepigwa marufuku kubeba bunduki kwa sababu hawezi kulenga shabaha inavyotakiwa.
Mtandao wa Huff Post umesema mkuu huyo Thomas
Bennett amepunguziwa majukumu yake ya upolisi baada ya kufeli mtihani
wake wa kulenga shabaha hivi karibuni.
Hatua hiyo inamaanisha polisi huyo haruhusiwi
kuwasha taa za kimulimuli za gari ya polisi (SIRENS) na pia hata
kusimamisha magari ya raia kwa ajili ya ukaguzi wa kawaida wa
barabarani.
Hata hivyo Polisi Bennett mwenyewe amedai kuwa
bado nana uwezo wa kutekeleza majukumu yake kama kawaida. Afisa mtendaji
wa mji huo wa North Carolina Gregg Whitehead amesema bwana Bennett
ametakiwa kujiandaa kufanya majaribio mengine tena ya kulenga shabaha
kama inayotakiwa kipolisi.
Na kwa taarifa yako......Kuna takriban nywele mia tano hamsini katika kila nyusi za binaadam.
Tukutane wiki ijayo..... panapo majaaliwa...