Friday, March 30, 2012

Matokeo ya kura Ubungo yalikuwa na kasoro adai msimamizi

Matokeo ya kura Ubungo yalikuwa na kasoro adai msimamizi  Send to a friend
Thursday, 29 March 2012 21:05
James Magai
ALIYEKUWA Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi katika Jimbo la Ubungo, katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 amekiri kuwa kulikuwa na upungufu katika matokeo ya jumla ya jimbo hilo na kwamba dosari hakustahili  kusaini wala kuyatangaza matokeo.

Msimamizi huyo msaidizi, Gaudence Kadiarara, pia  alikiri kuwa Mbunge wa Ubungo, John Mnyika, aliingiza kompyuta zake ndogo katika chumba cha kuhesabia kura na kwamba walilalazimika kuachana na mfumo wa Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa ulikuwa unachelewesha matokeo.

Kadiara ambaye pia ni Ofisa Maendeleo na Ustawi wa Jamii katika Manispaa ya Kinondoni, alikuwa akitoa ushahidi katika kesi ya  kupinga matokeo ya uchaguzi  katika jimbo hilo.

Kesi hiyo ya kupinga matokeo yaliyompa ushindi Mnyika,  imefunguliwa na aliyekuwa mgombea mwenzake kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Hawa Ng’humbi.
Katika kesi hiyo inayosikilizwa Jaji Upendo Msuya, Ng’humbi anadai kuwapo kwa ukiukwaji mkubwa wa taratibu na sheria ya uchaguzi.

Katika ushahidi wake, Ng’humbi na mashahidi wake pia wanadai kuwepo kwa dosari katika matokeo kwa madai kuwa fomu ya matokeo ya jumla iliyopokewa na mahakama ina kura hewa 14,854, ambazo hazijulikanai zilikotoka.
Pia wanadai kuwa Mnyika alipeleka kompyuta zake katika chumba cha kujumlishia kura na kwamba aliingia na wafusi wake zaidi ya wanane katika chumba hicho, jambo ambalo ni  kinyume cha sharia.

Wanadai kuwa kwa pamoja, watu hao walimshinikiza aliyekuwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Rajabu Kiravu, aruhusu kutumia kompyuta hizo katika kujumlishia kura, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.
Akihojiwa na wakili wa upande wa madai, Issa Maige jana, shahidhi alikiri kuwa takwimu zinazoonekana katika fomu o ya matokeo si sahihi na kwamba

kwa mujibu wa matokeo, kura halisi zilikuwa ni 119823, kura halali zilikuwa ni 117,639 huku kura zilizokataliwa (zilizoharibika) zikiwa ni 2184.

Alidai kuwa Ng’humbi alipata jumla ya kura 5,0544 na Mnyika kura 66,742 na wagombea wengine 14 walipata kura 15,207 kwa pamoja akiwamo mgombea wa CUF, Julius Mtatiro, aliyepata kura 12,964.
Kwa fomu hiyo jumla ya kura za Ng’humbi na za Mnyika tu ni 117,286 karibu sawa na kura halali bila kujumlisha za wagombea wengine.
Awali akiongozwa na Wakili Mkuu wa Serikali kutoa ushahidi wake, shahidi huyo wa kwanza wa upande wa wadaiwa, alikiri kuwapo kwa upungufu katika fomu hiyo ya matokeo.

 “Tatizo hapa ni kwamba kura halisi ni pungufu ya kura walizopata wagombea wote, kwa hiyo hili ni kosa. Nikiziangalia kwa harakaharaka hizi kura halisi (zinazooneshwa kwenye fomu hizo) ni za vyama vya CCM na Chadema tu,” alidai shahidi huyo.
 Alidai kuwa katika kujumlisha, walishughulika zaidi na kura za wagombea wa CCM  na Chadema kwa kuwa ndivyo vyama ambavyo vilikuwa vikijirudiarudia kila mara katika kura.
Alipoulizwa na Jaji Msuya kuhusu kura za vyama vingine kutokujumlishwa, shahidi huyo alijibu, “ndilo kosa lililofanyika,” .

Akijibu swali la Wakili wa Serikali juu ya  kura za vyama vingine kutohesabiwa, alijibu kuwa ni tatizo la kibinadamu na kwamba kura zao zote zipo.

Shahidi huyo alilazimika kufanya mahesabu upya, ili kujibu swali la Jaji Msuya aliyetaka kujua idadi ya kura za wagombea wa vyama vyote.

Baada kufanya hivyo, alijibu kuwa kura halali zilipaswa kuwa 132,496, badala ya 117,639 zinazoonekana kwenye fomu  na kwamba kura halisi zilipaswa kuwa 134,680 badala ya  119,823.

Sehemu ya mahojiano baina ya shahidi huyo na Wakili Maige ilikuwa kama ifauatvyo:
Wakili Maige: Shahidi nani alijaza fomu hiyo (namba 24B ya matokeo ya jumla ya ubunge).

Shahidi: Ni msimamizi msaidizi mwenzangu Sioni.
Wakili: Mli-cross check accurancy ya recording mlizoziweka katika fomu hiyo?
Shahidi: Ndio
Wakili: Kwa hiyo dosari hizo mlizijua tangu mwanzo na ninyi ni sehemu ya dosari hizo?

Shahidi: Hatukuzifahamu kabla, tungezifahamu tungeweza kuzirekebisha.
Wakili: Kwa jinsi hiyo fomu ilivyo, msimamizi angebaini kuwa kuna kura hewa zaidi ya 14,000 katika 24B angesaini?
Shahidi: Asingesaini.

Wakili: Asingesaini kwa sababu matokeo yaliyorekodiwa si halali na sahihi, kweli si kweli?
Shahidi: Kimya

Jaji Msuya: Kwa hiyo asingesaini kwa sababu hayako sawa sawa?
Shahidi: Ndio mheshimiwa jaji.
Akizungumzia jukumu lake katika chumba cha kujumlishia kura, shahidi huyo alidai kuwa lilikuwa ni kusoma  matokeo kutoka kwenye fomu za matokeo ya vituoni na kumwezesha  karani kuyaingiza kwenye kompyuta na kujumlisha.

Akizungumzia madai ya Mnyika kupeleka kompyuta zake tano  kuhesabia kura, alikiri kuwa alipigiwa simu akiwa nje kuwa Mnyika alipeleka  kompyuta zake na kwamba hata hivyo alipofika ofisini hawakuzitumia.

Alidai kuwa kompyuta hizo zilitumiwa na Mnyika na kwamba wao walitumia kompyuta (laptop).
Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa wakiwa katika chumba cha majumuisho Mnyika alimweleza msimamizi msaidizi wa Uchaguzi Lambaert Kyaro kuwa watumie kompyuta zake kwa katika kujumlisha kura kwa kuwa kompyuta za Tume ya Uchaguzi(NEC) zilikuwa zinachelewesha kiasi kwamba wangeweza utumia hata siku 15.


Shahidi huyo aliendelea kudai kuwa alimfuata Kiravu na kupinga matumizi ya kompyuta za Mnyika lakini wale wafausi wa Chadema waliendelea kumzongazonga wakimfuata kila mahali wakimshinikiza akubali kutumia kompyuta za Mnyika hadi Kiravu akakubali.

No comments:

Post a Comment