Tepe za HIV shuleni Tanzania zakera
15 Machi, 2012 - Saa 13:28 GMT
Wanaharakati nchini Tanzania
wameelezea kughadhabishwa na hatua ya baadhi ya shule nchini humo
kuwataka wanafunzi wanoishi na virusi vya HIV kuvaa riboni nyekundu
kwenye sare zao za shule wakiwa shuleni.
Mwalimu mkuu wa shule moja ameambia BBC kuwa
kitendo hicho kilifanyika kufuatia ombi la wazazi kuhakikisha kuwa
wanafunzi wagonjwa hawapewi majukumu ambayo huenda yakaathiri afya yao.Lakini ubaguzi kama huu unakiuka sheria ambao adhabu yake ni kifungo cha miaka mitatu gerezani kulingana na shirika moja la kutetea haki za waathirika wa HIV.
Waziri wa afya amesema hawezi kutoa tamko lolote kuhusu madai hayo hadi uchunguzi utakapofanywa.
Kulingana na shirika la UNAids, takriban asilimia tano ya watu milioni 1.4 nchini Tanzania, wanaishi na virusi vya HIV.
No comments:
Post a Comment