Rais Karzai asema NATO iondowe askari
15 Machi, 2012 - Saa 16:11 GMT
Rais Hamid Karzai wa Afghanistan
amelitaka Shirika la kujihami la NATO lirejeshe vikosi vyote vya
Kimataifa vilivyo nchini mwake ndani ya vituo vyao.
Ombi hilo alilolitoa wakati wa mazungumzo na
Waziri wa Marekani wa Ulinzi, Leon Panetta mjini Kabul linatokea siku
tano baada ya askari wa vikosi vya Marekani kuwaua raia 16 wa
Afghanistan wakiwa nyumbani kwao. Kutoka Kabul, Hii hapa taarifa ya
Quentin Somerville:)Rais Karzai amemuomba Wazir wa Ulinzi wa Marekani arejeshe vikosi vya Kimataifa katika kambi zao zilizoko nchini Afghanistan, na kukomesha ulinzi wa doria katika vijiji na miji. Amesema kua vikosi vya Afghanistan vina uwezo wa kutekeleza majukumu hayo.
Bado hatua ya kusimamisha shughuli za vikosi hivyo vya Kimataifa ambavyo vilitazamiwa kurejea ndani ya kambi zao ifikapo mwisho wa mwaka 2013.
Katika tukio la kipekee kundi la Taliban limetangaza kua linasitisha mazungumzo na Marekani yaliyopangwa kwa nia ya kuunda afisi ya kisiasa katika Taifa la Ghuba la Qatar pamoja na mpango wa kubadilishana wafungwa.
Taliban wamelaumu matukio haya kwa masharti ya Marekani yasiyokubalika. Ilidhaniwa kua mpango wa kubadilishana wafungwa watano wa Taliban walioko katika gereza la Guantanamo na askari wa Marekani aliyetekwa nyara utafanyika matika majuma machache yajayo.
Tamko hili ni pigo kwa juhudi za kuanzisha mazungumzo ya amani na wakereketwa hao.
Duru za wanabalozi wa Marekani zinasema kua Taliban waliambiwa kua serikali ya Afghanistan sharti iwe sehemu ya majadiliano. Hilo ndio lililozua ubishi wa Taliban ambao hawamtambui Rais Karzai.
No comments:
Post a Comment