ICC kutoa hukumu dhidi ya Lubanga leo
14 Machi, 2012 - Saa 03:48 GMT
Kiongozi wa zamani wa waasi,
huko Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, Thomas Lubanga Dyilo leo hii
atajua hatima yake kufuatia mashitaka kadha yanayomkabili, yakiwemo ya
kuwatumia askari watoto katika jeshi lake.
Bw Lubanga anatuhumiwa kuongoza wapiganaji wa kabila la Wahema katika makabiliano ya wenzao Walendu katika vita vilivyotokea miaka kumi iliopita katika mkoa wa Ituri.
Muasi huyo amekanusha mashtaka yanayomakabili na anasisitiza kuwa yeye alikuwa mwanasiasa na sio mpiganaji.
Makundi yakutetea haki za binadamu yanasema utafiti wao umeonyesha kuwa zaidi ya watu elfu 60 waliuawa katika vita hivyo katika eneo la Ituri ambapo Thomas Lubanga alikuwa na ngome yake.
"Utafiti wetu unaonyesha kuwa uhalifu wa kivita ulitendeka, wanawake walibakwa, watu waliteswa na wengine walizuiliwa bila kufanya makosa yoyote wakati wa vita hivyo vya kikabila. Ni matumaini yetu kuwa hukumu ya leo itakuwa ishara kuwa haki itatendeka" alisema Bi Anneke Van Woudenberg wa shirika la Human Rights Watch.
Thomas Lubanga ndio kiongozi aliyefunguliwa mashataka lakini mwenzake Jenerali Bosco Ntaganda bado hajachukuliwa hatua zozote na anatumikia jeshi la DR Congo.
Kesi hii imedumu kwa muda mrefu na hukumu hii inasubiriwa kwa hamu ni wakaazi wa Ituri ambao bado wanamakovu ya vita hivyo.
No comments:
Post a Comment