Filamu ya Kony yasitishwa Uganda
15 Machi, 2012 - Saa 10:18 GMT
Vuguvugu linaloonyesha kanda
ya video kuhusu kiongozi wa kundi la waasi la LRA, Joseph Kony,
imesitisha maonyesho ya kanda hiyo kaskazini mwa Uganda.
Filamu hiyo ya nusu saa, iitwayo ''Ivisible
Children'' ilitengezwa na wanaharakati nchini Marekani kushinikiza
viongoziwa dunia kumkamata kiongozi huyo wa waasi Joseph Kony. ,Filamu yenyewe imekuwa enye kutizamwa sana kuliko zote kwenye mtandao wa You Tube, tangu kutolewa kwake wiki jana. Imetazamwa na watu milioni 78 wiki jana pekee.
Lakini ilipoonyeshwa kwa mara ya kwanza mjini Lira, maelfu ya wenyeji walishikwa na hasira baada ya kuitizama.
Wengi miongoni mwa waliokuwa wanaitizama filamu hiyo, waliwahi kuteswa na waasi wa Kony na hivyo kuhisi kwamba iliwagusa sana.
Kundi la LRA, linasifika kwa kuwateka nyara watoto, kuwalazimisha watotowavulana kutumika kama wanjeshi na kutumia watoto wasichana kama watumwa wa ngono.
No comments:
Post a Comment