George Cloony akamatwa kuhusu Sudan
16 Machi, 2012 - Saa 18:03 GMT
Gwiji wa sinema, George Clooney amekamatwa kuongoza maandamano nje ya ubalozi wa Sudan mjini Washington DC nchini Marekani
Muigizaji huyo alikuwa anashiriki maandamno
yaliyopangwa kutahadharisha dunia kuhusu tisho la kuzorota kwa hali ya
kibinadamu katika eneo lenye mapigano mpakani mwa Sudan na Sudan Kusini.
Babake Cloony, Nick, pia alizuiliwa wakati wa maandamano hayo.
George Clooney ni mtetezi mkubwa kuhusu maswala ya Sudan. Amefanya ziara nyingi tu nchini humo.
Muigizaji huyo maarufu wa Hollywood, babake pamoja na wakereketwa wengine, walikamatwa na kufungwa pingu mikononi baada ya kukataa kutii maagizo ya polisi kuondoka kutoka ubalozi huo.
Wengine waliokamatwa ni pamoja na Martin Luther King wa tatu, mbunge wa deomcrat wa jimbo la Massachusetts Jim McGovern na mbunge wa Virginia Jim Moran.
No comments:
Post a Comment