Watu milioni 15 wakabiliwa na njaa Sahel
29 Machi, 2012 - Saa 03:11 GMT
Mkurugenzi wa Opareshini anayeshughulikia maswala ya kibinadam amelitaja eneo hilo kuwa ni janga la kimataifa.
Umoja wa Mataifa umesema kuwa mamilioni ya watu katika eneo la Afrika la Sahel lililokumbwa na baa la njaa wanakabiliwa na upungufu wa chakula uliosababishwa na ukame na migogoro, na mipango ya kuwapatia msaada ni chini ya asilimia 40 ikitolewa kwa ajili ya kukabiliana na hali itakapofikia kilele chake.
Sahel ni eneo lenye nchi karibu kumi na mbili zikiwa maskini kuliko zote kusini mwa jangwa la Sahara.
John Ging amesema watu milioni 15 wameathiriwa na tatizo la ukoefu wa chakula.
Akizungumza baada ya kutembelea nchi za Niger, Burkina Faso na Mauritania,
amesema tayari huu ni mgogoro kwa upande wa ukubwa wa tatizo lenyewe na kiwango cha mateso ya binadamu na litakuwa baya zaidi, la ivyo mipango ya kukabiliana nalo inatengewa fedha za kutosha.
Ni suala la kufa au kupona kwa mamilioni ya watu walio katika janga hilo.
Bwana Ging amesema mwaka huu mamilioni wa watu katika eneo la Sahel siyo tu wamekosa mvua lkini madhara yake baada ya vita vya Libya, hofu kutoka mapigano ya Nigeria kati ya serikali na kikundi cha Boko Haram na hivi karibuni mapinduzi ya kijeshi nchini Mali.
No comments:
Post a Comment