Wednesday, March 28, 2012

MWANACHUO ALIEMTUKANA FABRICE MUAMBA KWA KUANGUKA UWANJANI AHUKUMIWA KWENDA JELA.

MWANACHUO ALIEMTUKANA FABRICE MUAMBA KWA KUANGUKA UWANJANI AHUKUMIWA KWENDA JELA.

2
.
Mwanachuo wa Uingereza Stacey Liam ambae aliandika kwenye twitter maneno ya kibaguzi na matusi kwa mchezaji Fabrice Muamba wa Bolton muda mfupi baada ya kuanguka uwanjani siku kumi zilizopita, amehukumiwa kwenda jela.
Stacey alipandishwa mahakamani wiki iliyopita na kukubali kosa baada ya kukamatwa na polisi ambao walipata taarifa za Liam kutoa maneno hayo ya kibaguzi kupitia kwa watu mbalimbali waliyoyaona kwenye twitter na kuchukizwa nayo.
The sun wamesema Adhabu ambayo alikua apewe ni miaka saba gerezani lakini jaji amesema mwanachuo huyo amehukumiwa kwenda jela kwa siku 56 (mwezi mmoja na siku kama 25) kwa kosa hilo.

No comments:

Post a Comment