M23 wakaribia Goma
18 Novemba, 2012 - Saa 12:39 GMT
Wapiganaji wa mashariki mwa
Jamhuri ya Demokrasi ya Congo wanasema wako katika vitongoje vya Goma,
mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini.
Jumamosi, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilitaka kundi la wapiganaji la M23 kuacha kuelekea mji wa Goma, na nchi nyengine ziache kulisaidia kundi hilo.
Katibu Mkuu, Ban Ki-Moon, alimsihi Rais Kagame wa Rwanda atumie madaraka yake kuwazuwia wapiganaji hao.
Rwanda inakanusha kuwa inawasaidia wapiganaji hao.
Naibu Katibu Mkuu wa shughuli za kuweka amani za Umoja wa Mataifa, Herve Ladsous, aliulizwa Jumamosi kama M23 wanasaidiwa na nchi nyengine katika mapambano yanayoendelea.
Alisema: "Hatuwezi kuthibitisha au kukanusha kama Rwanda ilihusika hasa na mashambulio hayo ya M23.
Lakini naweza kusema kuna ripoti kuwa washambuliaji wa M23 wana silaha na zana za kutosha."
No comments:
Post a Comment