Israel yalenga ofisi za Hamas Gaza
17 Novemba, 2012 - Saa 14:05 GMT
Jeshi la wanahewa la Israil
limeshambulia kwa mabomu ofisi ya waziri mkuu kutoka chama cha Hamas
pamoja na jengo la baraza la mawaziri kwenye ukanda wa Gaza, katika siku
ya nne ya mashambulio.
Wapalestina 39, wakiwemo watoto kadha, wameuwawa tangu mashambulio hayo kuanza siku ya Jumatano.
Wapiganaji wa Gaza wameendelea kurusha makombora dhidi ya Israil, baada ya kulenga miji ya Tel Aviv na Jerusalem hapo jana.
Hamas imeomba madawa kutoka nchi za Kiarabu.
Israel inasema mashambulio yake yameleta uharibifu mkubwa katika vituo vilioko chini ya ardhi ambako makombora ndiko yanakorushwa.
Waziri wa mashauri ya Nchi za Nje wa Tunisia, ambaye alitembelea eneo la Gaza Jumamosi, alitoa wito kwa viongozi wa Kiarabu - wataokutana baadae mjini Cairo - kumaliza kile alichoita uhasama wa Israel.
No comments:
Post a Comment