Nani asiyejua Kondom?
Kondom ya Utumbo wa Nguruwe
Nani asiyejua kazi ya Kondom?
Lakini unajua kifaa hicho ambacho siku hizo husambazwa bure kilianza lini na wapi?
Tarehe yenyewe haifahamiki lakini katika karne
ya 15 yaani miaka mia 6 iliyopita kondom zilikuwepo na zilikuwqa
zinatumika katika bara la Asia.
Miaka mia sita iliyopita Kondom nchini china zilikuwa nizatengenezwa kutumia utumbo au mbuzi au kondoo.
Matajiri walikuwa wakitumia Kondom zilizotengenezwa kwa karatasi ya hariri iliyopakwa mafuta.
Nako nchini Japan Kondom zilikuwa zikitengenezwa
kwa magamba ya kobe au pembe za wanyama . Naama pembe ilikuwa ikivaliwa
kama kondom..ni huko Japan, miaka mia 6 iliyopita.
Ni katiuka karne iliyopita , mwaka 1900 kondom
zilizotengenezwa kwa utumbo wa mbuzi na kondoo hata utumbo wa ngombe
zilianza kuenea duniani.
Enzi hizo ilikuwa inatumiwa kukinga magonjwa ya zinaa na kuzuia mimbia isiyotakikana.
.........
Ni kawaida kwa wanawake wengi wakati wa ujazito
kuanza kutapika , kuwa ni kichefu chefu ,kuhisi kisunzi au kizunguzungu ,
kujisikia mnyonge, hasa wakati wa asubuhi. Wazungu wanasema ni Morning
sickness.
Wataalam wanasema haina sababu moja. Lakini
wanakubali kuwa husababishwa na ongezeko la homoni hasa ya Estrogen
katika mwili wa mwanamkea ambayo inaweza kumuongezea , uwezo wa kusikia
harufu hasa mbaya. Kuongezeka kwa maji aina ya gastroline.
Na unafahamu kuwa mwanamume.Baba mwenye nyumba
pia anaweza kuwa na dalili hizo hizo za ujauzito yaani ?,
kizunguzungu,kutapika , kichef chefu , tumbo kufura na kuwa na hasira
kama mkewe?
Kwa wakati huu Mike Dowdall , bwana mwenye umri
wa miaka 25 kutoka Manchester Uingereza amefura tumbo, anatapika tapika ,
asubuhi, husikia kisunzi au kizunguzungu na anapenda kula vitu vichachu
kama maembe mabichi yalitiwa chumvi au pilipili.
Kwa wakati huu mpenzi wake Amanda Bennett ni
mjamzito. Dahili za Mike zilipoanza bi Amanada alichukulia kwamba mpenzi
wake ambaye wameishia naye miaka mitatu anamfanyia mzaha au stihizai
Eti anamuiga vile anavyo tapika, na kupenda kula kula.
Lakini madaktari kutoka Manchster wanasema Bwana Mike ana ugonjwa wa mimba bandia. Wao wanaita Couvade syndrome
huu sio uchawi , bali ni ugonjwa unaoweza
kuwapata wanaume. Tumbo kufura, kutapika tapika asubuhi, kuhisi
kizunguzungu na kupenda kula maembe ya liotiwa chumvi au pilipili.
Mike amekuwa na uja uzito bandia kwa wiki 33 na
kama vile tu akina mama walio na mimba , Mike ameongeza uzani au zaidi
ya kila 3 na sasa anajihisi mchovu kila mara, kuumwa na mgongo na kwnda
haja ndogo kila mara.
Madaktari hao wanasema ugonjwa huu unaweza
kusababishwa na ile hali kuwa wasiwasi unaposubiri mkeo kujifungua, au
pia kuwa karibu sana na mkeo.
Bi Amanda ambaye ana mimba ya wiki zaidi ya 34
sasa analazimika kumsugua mumewe mgongoni na kiunoni kila siku na
kumkanda tumbo lake.
Habari hizo zimeshamiri katika gazeti la The Sun la uingereza.
......
Si hadithi bali ni kweli kwamba , mtu na mkewe wakiishi kwa zaidi ya miaka 25 huishia kufanana!
Asante msikilizaji wa BBC kutoka Tanzania kutukumbusha hao?
ukitaka kuthibitisha hilo hebu mwaangalie bibi na babu, ukiwa wewe ni mtum mzima hebu waangalie wazazi wako wote wawili?
Mwalimu Nyerere
Hebu tazama picha ya Hayati baba wa Taifa wa Tanzania Mwalimu Julius Nyerere na Mama Maria? Unaonaje?
Mama Maria Nyerere
Lakini kitu gani kinasababisha hali hii ya mtu na mkewe kufanana baada ya kukaa pamoja kwa miaka 25 au zaidi?
Waalam wanasema , ikiwa kuna upendo kati yenu, hii itachangia?
kwa vile kwa miaka 25 mume na mke hucheka pamoja
, kulia pamoja,wakati wa hupata msiba uhuzunika pamoja , wakati wa
matatizo na mihangaiko wanakabiliana nayo pamoja michoro hivi vinasaidia
kugeuza shepu na sura au uso wa mtu hivyo mume na mkewe huishia
kufanana.
vyakula pia inasaidia kuwafanya wafanane. kwa
vile wamkaa pamoja kwa miaka , mume na mkewe hula vyakula aina moja na
kukaa mazingia aina moja hii pia inasaidi kuwafanya wafanane.
Ni utafiti uliofanywa na Dr. Zajonc(ZI-onz)
akishirikiana na Pamela Adelmann, Sheila Murphy na Paula Niedenthal na
kucahpiswha katika jarida la kisayansi la , Motivation and Emotion.
..........
Jee unataka kujua utakapozeeka utafanana vipi?.
Kazi rahisi sana.
Wataalam wakiongozwa na Dr. Zajonc(ZI-onz)
wanasema kama wewe nimwanamume hebu muangalie baba mkwe wako, na kama
wewe ni mwanamke , muangalie kwa umakini mama mkwe. Urefu unaweza kuwa
tofauti lakini sura, utakapozeeka utafanana kama wakwe zako.
.........
nani anataka dola milioni 64 bila kutoa jasho jingi?
nadhani kazi hii itakuwa nyepesi mno kwa jamaa wa Bongo Tanzania, au Mombasa, au Uganda mtuweza?.
Tajiri mmoja nchini Hong Kong ametoa zawadi ya
dola milioni 64 za kimarekani kwa mtu yeyote atakaye faulu kumtongoza
binti yake bi Gigi Chao na akubali kuolewa nae.
tatizo ni hili bi Chao ni msango, au lesbian mwanamkea nayependelea kufanya mapenzi ya jinsia moja.
tatizo jengine ni kuwa bi Chao mwenye umri wa miaka 33 tayari amefunga ndoa kisiri na mwanamke mwenzake hivi majuzi tu.
sasa basi, ukitaka dola hizo milioni 64 za
kimarekani mtongoze, Bi chao , ufaulu kumuondoa katika ndoa hiyo na
mwanamke mwenzake na uafaulu kumuoa.
kama unaweza basi niandike katika facebook, BBC swahili.com nikuunganisha na tajiri huyo wa Hong Kong
Jina langu ni Odhiambo Joseph tukutane katika
Internet BBCSWAHILI.COM katika Kisa na Mkasa au ungana nami wiki ijayo
Mungu akipenda.