Maiti Ya Gaddafi Yawekwa Kwenye Friza la Nyama |
Gaddafi muda mfupi baada ya kukamatwa |
Sunday, October 23, 2011 1:17 PM
Maiti
ya aliyekuwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi imewekwa kwenye
friza la nyama mjini Misrata na itaendelea kukaa humo kwa siku chache
zijazo ili kila mtu aamini kuwa Gaddafi ameuliwa. |
Mwili
wa aliyekuwa kiongozi wa Libya, Kanali Muammar Gaddafi umehifadhiwa
kwenye friza la depo la nyama mjini Misrata ambako waziri wa mafuta wa
Libya, Ali Tarhouni amesema kuwa itaendelea kuwekwa humo kwa siku kadhaa
ili watu wajue kuwa ni kweli Gaddafi ameuliwa.
"Nimewaambia wauweke mwili wa Gaddafi kwenye friza ili watu wajue ni kweli Gaddafi ameuliwa", alisema waziri huyo wa mafuta.
Gaddafi
aliuliwa kwenye mji alikozaliwa wa Sirte baada ya kukamatwa akiwa hai
alipojeruhiwa kutokana na mashambulizi ya majeshi ya NATO na baadae
mashambulizi ya wanajeshi wa baraza la mpito la Libya, NTC.
Kwa
kawaida maiti ya kiislamu hutakiwa kuzikwa ndani ya masaa 24 lakini hadi
sasa haijulikani ni lini Gaddafi atazikwa kwakuwa kuna mvutano ndani ya
NTC juu ya wapi Gaddafi azikwe.
"Hadi sasa hakuna uamuzi
uliotolewa juu ya mazishi ya Gaddafi" alisema Mahmud Shamam alipokuwa
akiongea na shirika la habari la AFP na kuongeza "Haijulikani kama kama
maiti ya Gaddafi itaendelea kuhifadhiwa mjini Misrata au kama
itasafirishwa sehemu nyingine".
Viongozi wa NTC hawajaafikiana
juu ya mazishi ya Gaddafi lakini hawataki kuona kaburi la Gaddafi
linatumika kama alama ya ukumbusho kwa wafuasi wa Gaddafi waliobaki.
Shirika
la habari la BBC limeripoti kuwa kuna mipango ya kufanya mazishi ya
Gaddafi yawe ya siri huku pia kukiwa na tetesi kuwa huenda Gaddafi
akazikwa baharini kama mazishi ya aliyekuwa kiongozi wa Al-Qaeda, Osama
bin Laden yalivyofanyika kwenye bahari ya Uarabuni. |
GONGA HAPA KWA PICHA ZA MAITI YA GADDAFI |
|
|
No comments:
Post a Comment