NATO inatamatisha opereshi zake Libya
31 Oktoba, 2011 - Saa 03:27 GMT
Operesheni za Nato nchini Libya zinatarajiwa kukamilika hii leo.
Mwezi wa Machi, baraza hilo lilitoa ruhusa kwa mbinu zozote zitumike kuwalinda raia.
Ruhusa hiyo ya Umoja wa mataifa ilifuatia hatua ya Kanali Muammar Gaddafi kuanza kuwashambulia waandamanaji waliokuwa wakipinga utawala wake wa miaka 42.
Katibu Mkuu wa Nato Anders Fogh Rasmussen amesema kuwa operesheni hiyo ilikuwa miongoni mwa zilizofaulu zaidi katika historia ya Nato.
Shambulio la kwanza la Nato lilitekelezwa tarehe 19 Machi, wakati majeshi ya Kanali Gaddafi yalikuwa yanakaribia mji wa Benghazi uliokuwa unashikiliwa na waasi.
Nato iliweza kuendeleza operesheni yake nchini Libya kutokana na usaidizi wa kivita kutoka Marekani.
Na Wakati Kanali Gaddafi alipotekwa, wengi walihoji ikiwa nia ya majeshi hayo na NATO yalikuwa kusaidia mageuzi na sio kulinda raia.
Hata hivyo katibu wa Nato anasema kazi yao huko Libya imekamilika baada jeshi lao kusaidia kuzuia mauaji ya halaiki na kuokoa maisha.
Wakuu wa baraza la mpito la kitaifa NTC wamelitaka jeshi la NATO liendelee kuwepo nchini Libya.
Marekani imesema suala hilo linajadiliwa hasaa kutokana uzoefu wa jeshi hilo kutekeleza mafundisho ya kijeshi na kuharibu silaha.